https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Tuesday, October 08, 2013

Mgomo wa mabasi yaendayo mikoani unaendelea, mabasi kadhaa yaonekana barabarani yakiendelea na kazi kama kawaida


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
JUHUDI za kutatua mgomo wa mabasi yaendayo mikoani zinaendelea, huku mabasi kadhaa yakionekana barabarani kuendelea na safari zao kama kawaida.
Kampuni ya mabasi ya Dar experess gari lake lilionekana barabarani, ikiwa ni baada ya kutokea taarifa za mgomo wa mabasi yaendayo mikoani leo.

Mabasi ya Abood, Happy Nation, Upendo, Dar Express yalionekana katika barabara ya Morogoro yakiwa na abiria kwa ajili ya kuendelea na safari zao.

Hata hivyo, kumekuwa na mvutano wa aina yake, sanjari na kukwamisha safari za mabasi mengi na kuwasumbua abiria katika safari zao.

Mgomo huo umekuja siku moja baada ya magari makubwa ya kubeba mizigo malori nayo kugomea asilimia tano kwa yale yatakayozidisha mizigo.

Uamuzi wa faini hiyo umetokana na kuwataka maderevaa wasizidishe uzito katika magari yao ili kulinda barabara zinazoweza kuharibiwa na mizigo.

Mgomo huo umesababisha baadhi yao wasitishe safari zao, ikiwa ni njia ya kuwafanya wasisumbuke katika stendi ya mabasi yaendayo mikoani Ubungi

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...