https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Sunday, October 20, 2013

Rais Kikwete alipozindua Chuo cha VETA cha wilayani Makete jana

Rais Jakaya Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Chuo cha VETA cha Wilaya ya Makete jana kilichojengwa katika Mji wa Iwawa, Makao Makuu ya wilaya hiyo. KatIka hafla hiyo uongozi wa Chuo hicho umeamua kukipa jina la Jakaya Kikwete kwa jitihada zake alizowezesha wilaya ya Makete kuwa ya kwanza nchini kuwa na chuo cha VETA cha wilaya. Kulia kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Elimu NA Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Makete Ndugu Josephine Matiro.
Rais Jakaya Kikwete akifuatana na Mkewe Mama Salma walipokitembelea Chuo cha VETA cha Makete na kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanachuo wa chuo hicho mara tu baada ya kukizindua rasmi jana.
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma wakipata maelezo ya namna gani ya kupata udongo unaofaa kwa ajili ya kufyatua matofali kutoka kwa Geofrrey Sanga na Abel Mbilinyi, wanachuo wa mwaka wa kwanza wa chuo hicho jana.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...