https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, October 10, 2013

Ziara ya Zitto Kabwe wilayani Uyui pichani akimwaga sera zake

Zitto Kabwe akihutubia umati wa wananchi Uyui jana.

Siku ya 5 ya ziara ya CHADEMA Kanda ya Magharibi imetufikisha Jimbo la Igalula, wilaya ya Uyui. Tumekutana na wananchi katika vijiji vya Goweko, Loya, Miswaki, Miyenze na Kigwa.

Tumezungumza kuhusu changamoto ya usafiri wa Reli, wafugaji kunyanyaswa na watendaji wa kata na askari kwa kunyanganywa mifugo, zao la Tumbaku, maji safi na salama na suala la jumla la Katiba na mchakato wa kuandika katiba.

Kimsingi shughuli za kiuchumi za wananchi ni kubwa na hasa Kilimo na mifugo. Hata hivyo ukosefu wa miundombinu unafanya wananchi wasipate thamani ya mazao yao na jasho la kazi zao.

Nilipofika Kijiji cha Loya nimeona eneo kubwa lina miti ya mihama. Wananchi wanatumia tu mihama wakati wa njaa na mara nyingi matunda haya yanaharibika tu. Lazima matunda haya yana matumizi yake ya kiviwanda maana ‘kernel’ yake ina mafuta.
Na hili ni swali aliloacha Mh Zitto Kabwe
Nani anajua matumizi ya Mihama?



Zitto akimwaga hoja wilayani Uyui jana.

Watu wakimsikiliza Zitto, Mbunge wa Kigoma Kaskazini ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Zitto Kabwe akiwa amebeba nazi kama anavyoonekana pichani.


No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...