https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Sunday, October 13, 2013

Yusuphed Mhandeni: Mazuri mengi yanakuja tawi la Yanga la Green Stone

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MLEZI wa Tawi la Yanga la Mwananyamala, Yusuph Mhandeni, maarufu kama Yusuphed Mhandeni, amesema mambo mazuri yanawekwa ili kulifanya tawi hilo liwe la aina yake.
Yusuphed Mhandeni kulia akijadili jambo la wanachama wa Yanga, Tawi a Green Stone, Mwananyamala. Picha na Makakta yetu.
 
Yusuphed ambaye ni mdau wa muziki na Mchumi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Makumbusho, alisema kuwa lengo lao ni kulipaisha tawi hilo nchi nzima.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mhandeni alisema kwamba hali hiyo inamfanya yeye kama mlezi aumize kichwa namna ya kulijengea uwezo zaidi tawi lao lililozinduliwa mapema mwaka huu.

“Huu ni wakati wa kukaa na kutafakari namna gani ya kulisaidia tawi hili la Green Stone na kuliweka juu zaidi kati ya matawi yote ya Yanga hapa nchini.
“Hili ni tawi lililozinduliwa mapema mwaka huu ila limesheheni mipango kabambe ya kuliimarisha na kuwa na uwezo wa juu katika ramani ya soka,” alisema.

Tawi hilo lipo chini ya mwenyekiti wake Lumolwe Matovolwa maarufu kama ‘Big’ anayetamba pia katika tasnia ya filamu hapa nchini na kupendwa na wengi.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...