https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Saturday, October 12, 2013

Francis Cheka aitwa wilayani MuhezaNa Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KOCHA wa masumbwi wilayani Muheza, mkoani Tanga, Charles Muhiru, amemwita bondia Fransic Cheka ili aende kuhamasisha mchezo huo wilayani humo.
Bondia Francis Cheka, pichani.
Cheka atakuwa wilayani humo ambapo pia kutakuwa na mapambano kadhaa kwa ajili ya kuhakikisha kuwa uwapo wake unakuwa na chachu kwenye ngumi.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka wilayani humo, Muhiru alisema kuwa Cheka ni miongoni mwa mabondia makini wenye uwezo wa aina yake hapa nchini.

Alisema jambo hilo linamfanya amualike mwanasumbwi huyo ili kuleta picha kamili kwa wadau wa ngumi na wenye hamu ya kuona mchezo huo unasonga mbele.

“Tumepanga Cheka awepo hapa kwenye Sikukuu ya Idd Pili katika viwanja vya Jitegemee, wilayani Muheza, mkoani Tanga ambapo siku hiyo kutakuwa na mapambano ya ngumi na yeye kuhamasisha.

“Naamini mpango huu utakuwa na tija kwa kiasi kikubwa kwa sekta ya masumbwi mkoani Tanga na Tanzania kwa ujumla, hivyo kila kitu kitakwenda sawa,” alisema.

Sio mara ya kwanza kwa Cheka kukaribishwa katika sehemu mbalimbali za Tanzania, ikiwamo katika Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, ikiwa ni njia ya kuthamini mchango wake katika tasnia ya masumbwi.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...