https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, October 04, 2013

Watanzania watatu kushiriki kozi ya waamuzi FUTURO III Addis Ababa

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WATANZANIA watatu ni miongoni mwa washiriki 30 walioteuliwa kuhudhuria kozi ya wakufunzi ya waamuzi ya FUTURO III itakayofanyika Addis Ababa, Ethiopia kuanzia Oktoba 5 hadi 10 mwaka huu.
Msemaji wa TFF, Boniface Wambura, pichani.
Msemaji wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa Leslie Leonard Liunda, Abdi Soud Mohamed na Israel Nkongo Mujuni ndiyo watakaoshiriki katika kozi hiyo itakayoendeshwa na wakufunzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Kozi hiyo pia itakuwa na washiriki kutoka nchi nyingine tisa za Afrika. Nchi hizo ni Gambia, Ghana, Kenya, Liberia, Nigeria, Seychelles, Sierra Leone, Somalia na Uganda.

Katika hatua nyingine, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Burundi kuchezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa wanawake chini ya miaka 20 Kanda ya Afrika kati ya Tanzania na Msumbiji.
Waamuzi hao watakaochezesha mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Oktoba 26 na 27 mwaka huu wataongozwa na Ines Niyonsara. Atasaidiwa na Jacqueline Ndimurukundo na Axelle Shikana.

Irene Namiburu kutoka Uganda ndiye atakayekuwa mwamuzi wa mezani wakati Kamishna wa mechi hiyo ni Evelyn Awuor wa Kenya. Mechi ya marudiano itachezwa jijini Maputo kati ya Novemba 9 na 10 mwaka huu, na itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar.

Fainali hizo za Kombe la Dunia zitafanyika mwakani nchini Canada, ambapo Tanzania inashiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo ya Kombe la Dunia kwa wasichana.

Timu ya Tanzania tayari imepiga kambi mkoani Pwani ikiwa chini ya Kocha wake Rogasian Kaijage.

Wachezaji walioko kambini ni Amina Ally, Amina Ramadhan, Amisa Athuman, Anastazia Anthony, Anna Hebron, Belina Julius, Donisia Daniel, Esther Mayala, Fatuma Issa, Gerwa Lugomba, Happiness Lazoni, Harriet Edward, Hellen Maduka, Irene Ndibalema, Jane Cloud, Khadija Hiza na Latifa Salum.

Wengine ni Maimuna Hamis, Mwanaidi Khamis, Najiati Abbas, Neema Paul, Niwael Khalfan, Rehema Abdul, Sabahi Hashim, Sada Ramadhan, Shamimo Hamis, Shelder Boniface, Stumai Abdallah, Tatu Idd, Therese Yona, Violet Nicholas, Vumilia Maarifa, Yulitha Kimbuya na Zena Said.  

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...