https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, February 28, 2014

Kila la kheri Yanga kesho dhidi ya Al Ahly ya Misri



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaitakia kila la kheri yake kwenye mechi yake ya kwanza ya raundi ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly kutoka Misri.

Mechi hiyo inachezwa kesho (Machi 1 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia 10 kamili jioni. Timu hizo zitarudiana Machi 9 mwaka huu jijini Cairo, Misri.

Maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika ambapo kamishna Abbas Sendyowa kutoka Uganda na waamuzi wanne kutoka Burundi tayari wapo nchini kwa ajili ya mechi hiyo inayotarajiwa kuvuta maelfu ya washabiki.

Milango yote katika uwanja huo itakuwa wazi, ukiwemo ule wa upande wa Uwanja wa Ndani (Indoor Stadium) wakati Barabara ya Taifa (Taifa Road) itafungwa kuanzia chuo cha DUCE hadi msikitini kuanzia saa 4 asubuhi.

Magari maalumu yenye sticker pekee ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani. Vilevile washabiki wanakumbushwa kuwa hawaruhusiwi kuingia uwanjani wakiwa na silaha au vifaa vyovyote vya chuma.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...