Na Mwandishi Wetu, Handeni
WANANCHI wilayani Handeni, mkoani Tanga, wameaswa kulima
maza ya biashara na chakula ili kuwaondolea balaa la njaa linalowakumba kila
mwaka kutokana na kutegemea kilimo cha aina moja, yakiwamo mahindi.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, pichani.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Muhingo Rweyemamu
katika mahojiano maalum wilaya Handeni mkoani Tanga, ikiwa ni sera na mipango
kabambe ya kuweka sawa jambo hilo kwa maendeleo ya wananchi wa Handeni na
Tanzania kwa ujumla.
DC Muhingo alisema kuwa wakazi wengi wa Handeni wanategemea
kilimo cha mahindi kama zao la biashara na chakula, jaambo linalowafanya kila
wakati watu wengi wakabiliwe na njaa na kuwafanya waishi kwa tabu wakati wote.
“Ofisi yangu inajitahidi kuwaelimisha wananchi wengi waone
ipo haja sasa ya kulima mazao mengi ya biashara, ukizingatia kuwa sasa wengi
wao wanategemea mahindi kama zao la chakula na baadaye huuza kwa mahitaji yao.
“Naamini yapo mazao mengi ambayo endapo yatalimwa kwa wingi,
mahindi yatahifadhiwa kwa ajili ya chakula wao na familia zao, maana suala la
njaa Handeni linatokea kwasababu kuna mapungufu mengi, hasa ya chakula kuwa
haba,” alisema.
Kwa mujibu wa Muhingo, elimu ya ziada kwa wananchi na
wakulima wote kwa ujumla inahitajika wilayani humo ili watu wazoee kulima mazao
mbalimbali, ukiwamo ufuta, maharage na mengineyo kwa ajili ya biashara na
kuweka akiba ya chakula kwa zao la mahindi.
No comments:
Post a Comment