
Na Nathaniel Limu, Singida
JESHI
la Polisi mkoa wa Singida limefanikiwa kukamata vipande 16 vya meno ya
ndovu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 17.
Meno
hayo yamekamatwa siku nne (12/2/2014) toka meno mengine vipande 21
vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 43 milioni, kukamatwa kwenye eneo
lile lile la kizuizi cha mazao kilichopo katika kijiji cha Ukimbu kata
ya Mgandu wilaya ya Manyoni.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake, Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa
Singida.SSP.Cordula Lyimo amesema meno hayo yamekamatwa febr.16 saa tano
usiku huko katika kizuizi cha mazao kilichopo katika kijiji cha
Ukimbu,kata ya Mgandu tarafa ya Itigi wilaya ya Manyoni.
Alisema
askari wakiwa katika kizuizi hicho,walifanya ukaguzi kwenye gari T.288
AJF aina ya scania mali ya kampuni ya super service likiendeshwa na
dereva Ally Hamadi, likitokea Makogorosi Chunya,likielekea Itigi wilaya
ya Manyoni.
“Baada
ya upekuzi huo,walikuta meno hayo yakiwa yamehifadhiwa ndani ya begi la
nguo na kuwekwa kwenye keria za ndani ya basi.Mtuhumiwa aliweza
kupatikana wakati akiwa katika juhudi za kutaka kutoka nda ya basi ili
akimbie”,amesema Lyimo.
Kaimu
kamanda huyo,amesema uchuguzi zaidi unaendelea ili kubaini au kupata
mtandao kamili unaojihusisha na kuwinda pamoja na kununua nyara hizo.
No comments:
Post a Comment