Na Mwandishi Wetu, Kilindi
MKUU wa Wilaya Kilindi, Seleman Liwowa, amesema kwamba juhudi
za kukomesha migogoro inayoweza kuichafua amani kwenye wilaya hiyo mkoani
Tanga, inawekwa kwa kuhakikisha inawaweka sawa wakulima na wafugaji.
Mkuu wa wilaya Kilindi, Selemani Liwowa, pichani.
DC Liwowa aliuambia mtandao huu wa Handeni Kwetu kuwa
miongoni mwa migogoro hiyo tishio inasababishwa na wakulima na wafugaji, sanjari na ongezeko la watu wilayani humo na Tanzania kwa ujumla.
Alisema kuwa ofisi yake kwa siku kadhaa sasa imejaribu kukaa
na kuliangalia kwa kirefu suala hilo, hivyo anaamini watalipatia ufumbuzi kwa
manufaa ya Kilindi na Tanzania kwa ujumla.
“Tumegundua kuwa migogoro hii inasababishwa na wakulima na
wafugaji, huku chanzo pia kikiwa ni ongezeko la watu huku ardhi ikiwa haijapimwa.
“Nadhani tumekaa na kuona tupitie upya matumizi ya ardhi kwa
upande wa wakulima na wale wafugaji ili kuhakikisha kuwa utulivu unakuwapo
wilayani hapa,” alisema.
Kilindi inatokea ubavuni mwa wilaya ya Handeni, mkoani Tanga,
ambapo kwa sasa inaongozwa na DC wake Muhingo Rweyemamu, ndani ya Mkoa wa
Tanga, ambapo p/ia upo chini ya Chiku Gallawa.
No comments:
Post a Comment