MKUU
wa Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest
Mangu pichani, ameanza kufanya mabadiliko ya baadhi ya makamanda wa mikoa, wakuu
wa upelelezi wa mikoa, wakuu wa usalama barabarani wa mikoa pamoja na
watendaji wengine wa vikosi na vitengo mbalimbali ndani ya Jeshi hilo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Advera Senso-SSP; miongoni mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa
mabadiliko ni pamoja na aliyekuwa Kamanda wa Mkoa wa Ruvuma Kamishna
msaidizi mwandamizi (SACP) Deusdedit Nsimeki anayekwenda kuwa Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Manyara, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara
Kamishna msaidizi (ACP) Akili Mpwapwa sasa anakuwa Kamanda wa Polisi
Ruvuma.
Taarifa hiyo imeeleza aliyekuwa Ofisa Mnadhimu Mkoa wa Lindi, Kamishna
Msaidizi (ACP) Renatha Mzinga anakuwa Kamanda wa Mkoa wa Lindi,
aliyekuwa Ofisa Mnadhimu Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi (ACP) Suzan
Kaganda amehamishwa kuwa Kamanda Mkoa wa Tabora huku aliyekuwa Kamanda
wa Polisi Tabora (ACP), Peter Ouma amehamishiwa Polisi Makao Makuu.
Wengine
ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mtwara, (ACP)
Eliyakimu Masenga anakwenda kuwa Mkuu wa Upelelezi Kikosi cha Tazara,
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Tabora (ACP) David Mnyambuga anakwenda kuwa
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Ilala, na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa
Ilala, (ACP) Juma Bwire, anakwenda kuwa Ofisa Mnadhimu Mkoa wa Tabora.
Aidha, aliyekuwa Ofisa Mnadhimu Mkoa wa Tabora Mrakibu Mwandamizi wa
Polisi (SSP) John Kauga anakuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Tabora,
aliyekuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Rombo (SSP) Mrakibu Mwandamizi, Ralph
Meela anakwenda kuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mtwara na aliyekuwa Mkuu
wa Upelelezi Kikosi cha Tazara, Mrakibu wa Polisi (SP) Isack Msengi
anakuwa Kaimu Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Pwani.
Katika
mabadiliko ya wakuu wa Polisi wa mikoa Usalama Barabarani; aliyekuwa
Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni (SSP), Ibrahim Mwamakula amehamishiwa
Trafiki Kanda Maalum Dar es Salaam, Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Mtwara
(SP), Awadh Haji anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni, na
(SP), Ezekiel Kiko Mgeni aliyekuwa Ofisi ya RPC Temeke, anakuwa Mkuu wa
Trafiki Mkoa wa Temeke.
Wengine
ni aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi Mrakibu wa Polisi (SP) James
Kiteleki anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Njombe, aliyekuwa Mkuu
wa Trafiki Mkoa wa Ilala, Mrakibu wa Polisi (SP) Meloe Buzema anakwenda
kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi, aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Trafiki Mkoa
wa Temeke Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Prackson Kibogoyo anakwenda
kuwa Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Pwani, na aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa
wa Njombe, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Chacha Nsaho Maro anakwenda
kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Ilala.
Hata hivyo taarifa hiyo imefafanua kuwa mabadiliko hayo ni ya kawaida
kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi katika
kuhakikisha kwamba wananchi wanaendelea kupata huduma bora ya usalama.
No comments:
Post a Comment