https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Wednesday, February 05, 2014

TANAPA yakabidhi madarasa mawili shule ya sekondari Nkoarisambu wilayani Arumeru

Mwenyekiti wa kamati ya ardhi,maliasili na mazingira ,Mh James Lembeli akiongoza ujumbe wake kusalimiana na wanachi wa kata ya Nkoarisambu katika wilaya ya Meru mkoani Arusha ambako kamati hiyo ilitembelea shule ya sekondari Nkoarisambu kuzindua majengo mawili ya madarasa.
Naibu waziri wa ardhi,maliasili na mazingira,Mahamud Mgimwa akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar kabla ya uzinduzi wa madarasa yaliyojengwa kwa mchango wa wananchi na TANAPA.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Nkoarisambu iliyopo wilayani Meru mkoani Arusha ambayo imejengewa madarasa mawili kwa ushirikiano wa wananchi na TANAPA.
Mwenyekiti wa kamati ya ardhi,maliasili na mazingira,Mh James Lembeli akijaribu kubadilishana mawazo na naibu waziri wa maliasili na utalii,Mahamud Mgimwa pamoja na mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassar.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mwilongo akizungumza wakati wa uzinduzi wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa msaada wa Nguvu ya wananchi wa Arumeru na shirika la hifadhi ya taifa ,TANAPA.
Mwenyekiti wa kamati ya ardhi,maliasili na mazingira,Mh James Lembeli akiwasalimia wananchi wa Arumeru wakati wa uzinduzi wa  wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa msaada wa Nguvu ya wananchi wa Arumeru na shirika la hifadhi ya taifa ,TANAPA.
Jengo lenye madarasa mawili ambalo limejengwa kwa nguvu ya wananchi wa Arumeru pamoja na shirika la hifadhi ya taifa TANAPA katika shule ya sekondari Nkoarisambu.
Naibu waziri wa maliasili na utalii,Mahamud Mgimwa akizungumza katika uzinduzi wa madarasa mawili ykatika shule ya sekondari ya Nkoarisambu wilayani Arumeru.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la hifadhi ya taifa TANAPA,Allan Kijazi akitoa taarifa ya kukabidhi mradi wa ujenzi wa madarasa mawili ,shule  ya sekondari Nkoarisambu wilayani Arumeru.

Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi,maliasili na mazingira Mh James Lembeli akizindua mradi wa ujenzi wa madarasa mawili ,shule ya sekondari  Nkoarisambu wilayani Arumeru,ujenzi ulifanywa kwa msaada wa shirika la hifadhi ya taifa(TANAPA)na wananchi wa Arumeru.

Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi,maliasili na mazingira Mh James Lembeli akizindua mradi wa ujenzi wa madarasa mawili ,shule ya sekondari  Nkoarisambu wilayani Arumeru,ujenzi ulifanywa kwa msaada wa shirika la hifadhi ya taifa(TANAPA)na wananchi wa Arumeru.
Mbunge wa jimbo la Arumeru mashariki Mh Joshua Nassar akizungumza jambo na mwenyekiti wa kamati ya ardhi,maliasili na mazingira Mh James Lembeli,kulia kwake ni mjumbe wa kamati hiyo Mh Henry Shekiff.
Mbunge wa jimbo la Arumeru mashariki Mh Joshua Nassari akizingumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa madarasa mawili ,shule ya sekondari Nkoarisambu wilayani Arumeru,ujenzi ulifanywa kwa msaada wa shirika la hifadhi ya taifa(TANAPA)na wananchi wa Arumeru.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...