https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, February 01, 2014

Mvutano juu ya kusudio la kijiji cha Misima, wilayani Handeni mkoani Tanga kuingizwa kwenye Halmashauri ya Mji wa Handeni

Mjadala huu umeandikwa na mwananchi wa kijiji cha Misima, Rashid Hassani Kilo, kama alivyouweka katika ukurasa wake wa facebook.

Rashid Hassan Kilo, mchambuzi wa mjadala huu. Umewekwa hapa ili kuwapa fursa wananchi wote kusoma mawazo haya na namna mchakato huo wa Misima kuingizwa kwenye Halmashauri ya Mji wa Handeni, wilayani humo mkoani Tanga. Hata hivyo, serikali kwa kupitia Mkurugenzi wa Mji wa Handeni, Thomas Mzinga, alituthibitishia blog hii kuwa mchakato huo ulifuata sheria zote na ni sehemu ya kimaendeleo ya wilaya nzima.

Habari za mchana huu wana Handeni? Kwa niaba ya watu wa kijiji cha Misima, nauleta kwenu mjadala wa uthibitisho kuwa Kijiji cha Misima hakikushirikishwa kabisa ktk mchakato mzima wa kuwa ndani ya Halmashauri ya mji wa Handeni.

Ni kwamba mnamo 23/04/2009, kupitia TBC-TAIFA, taarifa ya habari ya saa 2 usiku tumesikia tarifa juu ya kijiji chetu kuwa miongoni mwa vijiji vinavyounda mji wa Handeni.

Hatubishi kuwa ni maendeleo ila si mnakaa na kutathmini faida zake na hasara zake ili mizani izidi kwenye faida? Leo huu mkutano uliotoa muhtasari huo umefanyika wapi?

Tar 26/04/2009, majira ya saa 2 usiku tukatafutana watu kama 6 kwenda nyumbani kwa mw/kiti wa kijiji wakati huo mzee ZAKARIA MOHAMMED DOYO, kumuuliza juu ya taarifa hizi, nae alikiri kusikia radioni ila hajui imekuwaje? Lkn akatuahidi kuitisha mkutano 01/05/2009 ili tujadiliane. Tumesubiri hakuna kilichofanyika zaidi ya yy kutorokea kwenye migodi ya madini ya MOHAMMED ADAM HADJI.

Ilipofika tarehe ya ahadi bila mafanikio tukaenda kwa mw/kiti wa ccm kata ya Misima ili amshurutishe baada ya kukutana nae akamwambia ataitisha mkutano huo 06/05/2009, lakini pia hakuitisha. Wakati wote yakifanyika haya hatukuwa na kumbukumbu tukaona sasa tundikane wengi na tifuate taratibu na kuchagua watu wachache watakao fuata ngazi husika, ktk watu waliochaguliwa nilikuwa mmoja wao.

Tarehe hiyo hiyo 6 tukaandika barua kwenda kwa WEO yaani mendaji kata wakati huo Ndg. ISMAIL MROPE ili amshurutishe VEO wakatio huo Bw. MAULID ISMAIL YUSUF amshauri mwenyekiti waitishe mkutano. Kweli WEO aliandika barua yenye Kumb. Na. WEO/MD/VOL-II/08/09 ilikuwa 08/05/2009, yenye anuani YAH: KUITISHA MKUTANO MAALUM WA KUFAFANUA AGENDA YA KIJIJI CHA MISMA KUINGIA KTK MAMLAKA YA MJI HANDENI SIKU YA 13/05/2009 saa 8:00 alasiri.

Angalia jibu la mwenyekiti katka barua yenye KUMB. NA. SER/KIJ/MS/VOL-1/09 na anuani isemayo YAH: KUTOITISHA MKUTANO MAALUM WA KUFAFANUA AGENDA YA KIJIJI CHA MISMA KUINGIA KTK MAMLAKA YA MJI SIKU YA 13/05/2009 saa 8:00 alasiri.
Sababu za kutoitisha mkutano huo ni kwamba sijawahi kutoa ahadi kwa watu eti niwaitishie mkutano wa hadhara kwa ajili ya kuzungumzia agenda ya mji. Kwa kawaida mikutano huandaliwa na serikali si kwa mamlaka ya watu wachache. "Japo ilikuwa inaendelea ila point mmeziona" Mwisho akatia sahihi na kuandika jina lake ZAKARIA MOHAMMED DOYO.

Baadae zikatokea hujuma hali iliyopelekea mtendaji kata kuhamishwa haikuishia hapo mw/kiti wetu alienda hadi kituoni ili tujetukamatwe lakini polisi wanajua kazi yao kwani hakuwa na sababu za msingi wakampuuzia.

Tulipita ngazi hadi mkowani bahati mbaya mkuu wa mkowa kipindi kile Ndg. SAID KALEMBO hatukumkuta na kuacha barua yetu wakati huo wakuu wa mikowa wote waliitwa bungeni.

Hata hivyo baada ya kuipata alikuja mpaka Handeni na kucha maagizo kwa mkuu wa wilaya wakati huo Ndg. SEIF MPEMBENWE nae akafanya nasi mkutano na akaomba mchakato wetu uishie mkowani na kutoa maagizo mkutano uitishwe na akaniomba nimpe barua za madai yetu, nilipiga copy asubuhi yake baada ya mkutano yaani 29/06/2009 nilimpelekea na kumkabidhi ofisini kwake.

Katika mlolongo wote huu hakuna hata siku moja tumekaa mkutano na kulijadili hili. Na hata huo muhtasari wa sisi kuomba ni wa kughushi na sahihi za majina waliitwa wanafunzi wa Misima Sekondari ndio walio saini. Maana muhtasari ulioko huko eti Misima tumeomba wenyewe!

Na sababu ya viongozi kufanya hivyo baada ya wao kuiuza ardhi ya Misima, sasa mnapotawaliwa na sheria ya mji, ardhi si mali ya mkutano mkuu wa kijiji ila ni mali ya kamishna wa ardhi wa mji na si kwa kulima na kufuga ila mipango miji tena. Jamani nina mengi hapa hayatoshi ila siku moja nitakuja unguruma kwenye vyombo husika labda waniuwe mapema kwa kutetea haki ya vizazi vya Misima na uridhi wao pekee ambao ni ardhi tu, uliobaki! Vingine vyote vimeporwa! Mchana mwema.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...