Mbunge
wa Ubungo ambaye ni mjumbe wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, John
Mnyika, pichani, ameitaka serikali kuondokana na kigugumizi cha kuwataja kwa majina vigogo
wa ujangili.
Akizungumza
na Waandishi wa habari, Mnyika alisema kabla ya kuanza kwa Oparesheni Tokomeza
sehemu ya pili ni ambayo inatajwa kuanza muda wowote kuanzia sasa, ni busara
serikali ikaweka wazi majina ya vigogo wanaohusika na biashara hiyo ambao
wanatajwa kuwa ni watendaji wa serikali.
Alisema
ni dhahiri kwamba serikali inawafahamu vigogo wa ujangili ambao wanadaiwa kuwa
ni watendaji wa serikali na viongozi wakubwa katika ngazi za vyama vya siasa na
watendaji wa serikali na kwa maana hiyo Opereseheni Tokomeza awamu ya pili
haitakuwa na jipya endapo majina ya wahusika hao hayatawekwa hadharani.
Alisema
katika Hotuba yake ya kufunga mwaka mwishoni mwaka jana, Rais Kikwete
alikaririwa akisema kuwa Operesheni Tokomeza ujangili awamu ya kwanza
ilifanikiwa kufichua mitandao ya ujangili ambao wengine ni watendaji wa
serikali, hivyo hakuna sababu ya kuendelea kuweka katika mabano majina yao.
“Ujangili
umekithiri, kwenye hotuba yake ya mwisho wa Mwaka, Rais Kikwete, alieleza kuwa
operesheni tokomeza imesaidia kufichua mtandao wa majangili ambao wengine ni
watendaji wa serikali, sasa basi kabla ya kuanza kwa awamu ya pili ya
operesheni tokomeza, ni vizuri kwanza vigogo ambao wanafahamika kwa majina
“majangili” wakatajwa majina wazi na kuchukuliwa hatua,” alisema Mnyika.
Mnyika aliongeza kuwa ili matatizo na
mapungufu yaliyojitokeza katika awamu ya kwanza yasijirudie tena, kuna haja ya
kutajwa kwa majina ya wahusike ili washugulikiwe wao pekee na mitandao yao
badala ya kuwalenga wananchi wasiokuwa na hatia.
Aidha
Mnyika ambaye pia ndiye mkurugenzi wa habari na mawasiliano wa chama cha
demokrasia na maendeleo (CHADEMA), alishauri serikali ya Tanzania kuiga mfano
wa nchi nyingine kwa kupiga marufuku kwa muda zoezi la uwindaji wa Tembo na
Faru katika vitalu kwani kuna watu wanaotumia uwindaji huo kuchangya uwindaji
haramu na halali.
“Ili
kuepusha wananchi wa kawaida kulengwa katika operesheni hii, kuna haja ya
majangili vigogo majina yao kuwekwa hadharani, kama serikali itaendelea kuona
kazi kutaja majina haya sidhani kama operesheni tokomeza awamu ya pili itakuwa
na tija zaidi ya manyanyaso na mateso ya raia wasiokuwa na hatia,” alisema.
Kuhusu
suala la mapato yanayopatikana katika maeneo ya hifadhi za taifa pamoja na kodi
inayotozwa miradi inayotekelezwa na mashirika, mnyika alisema ni jambo la aibu
kutoza kodi miradi ambayo inatekelezwa na mashirika ya umma, miradi ya kusaidia
jamii inayozunguka maeneo ya mashirika, kama kwa hapa Tanapa na maeneo
yanayozunguka hifadhi ya Tarangire.
Alisema
ni busara serikali isiongeze mzigo wa kodi ilikuwezesha kiwango kidogo cha
fedha kinachotoka kiweze kufikia miradi mingine zaidi kwa kuongeza kuwa
serikali haitendi haki kwa mashirika hayo kwani
miradi hiyo inalenga kufanya kazi ambayo kimsingi ilikuwa ifanywe na
serikali, kimsingi ilikuwa ifanywe na wananchi.
“Maeneo ambayo yanazungukwa na hifadhi kama
vile maeneo yanayozungukwa na migodi, wananchi wanatarajia kwamba kiwango cha
mapato kinachotokana na mazingira yao kirudi kwenye jamii, kwa hiyo ukiondoa
miradi ya kusaidia kama hii ya ujenzi ya madarasa kuna haja ya kwenye mapato
yanayotokana na vivutio vya utalii kuwa na mgao wa moja kwa moja kwenye
Halmashauri na kuziwezesha kuwa na bajeti kubwa”, alisema Mnyika.
Akitolea
mfano Hifadhi ya Tarangire ambayo kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014, ilikusanya
bilioni 9.7, sasa ukiangalia bajeti ya miradi ya jamii, ambayo ni 193 milioni
pekee haifiki hata asilimia 2.5 ya mapato ambayo yamepatikana kwa hiyo ni
lazima kuwa na mfumo ambao mapato makubwa zaidi zitaongezeka kama kodi ya
huduma ya kijamii, kodi ya makampuni kwa sababu makampuni nazo zinatengeneza
faida kubwa.
No comments:
Post a Comment