https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, February 01, 2014

Matukio pichani katika sherehe za kumpongeza Absalom Kibanda kwa kushinda kesi

 Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006 Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Rai, Bingwa, Dimba na The African, Absalom Kibanda, akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni hiyo, hawapo pichani katika hafla fupi ya kumpongeza ushindi wake katika kesi iliyokuwa inamkabili iliyodaiwa kuwa ni uchochezi juzi. Halfa hiyo ilifanyika katika ofisi za Kampuni hiyo, Sinza Kijiweni.
Absalom Kibanda kushoto akifurahia jambo kutoka kwa MC, Sidi Mgumia, ambaye ni mwandishi wa Gazeti la The African. Kulia kwa Sidi ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa New Habari, Hussein Bashe.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni hiyo, Hassan Bumbuli, Jonathan Tito, Kambi Mbwana, Grace Hoka na Mareges Paul wote wamesimama. Ilikuwa burudani kubwa, huku wakiangalia kinachojiri katika tukio hilo la aina yake katika hafla hiyo.
 Shughuli inaendelea hapa. Kila mmoja macho mbelee. Hongera bwana Abasalom Kibanda..
Weee madada wa New Habari hawa, Jenifer Ullembo kushoto na Zaituni Kibwana. Wote walikuwapo na kushuhudia kinachoendelea.
 Muda wa burudani ukafika, Kwaito kwa kwenda mbele.
Ukitaka umuuzi Mwani Nyangassa, Mhariri wa Michezo wa Gazeti la Mtanzania, kitu white hicho basi mnyime muziki. Atakutoa ndukiiiiiiiiii. Nyuma ya Mwani Nyangassa ni Esther Mbusi. Mwenye miwani ni baba shughuli, Absaol Kibanda, naye akionyesha ubora wake.....

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...