Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
MIMI ni miongoni
mwa watu walioshangaa mno, pale wanachama wa Yanga, walipompigia magoti Mwenyekiti
wao Yusuph Manji ili agombee tena nafasi yake baadaye mwaka huu.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, pichani.
Nilipowaona
nilishangaa. Walionyesha udhaifu mkubwa katika sekta ya mpira wa miguu nchini.
Manji ni mfanyabiashara mwenye mapenzi na klabu hiyo tangu zamani. Hilo
linajulikana. Hivyo hata kutangaza kwake kutowania nafasi hiyo ni uungwana
mkubwa.
Kutangaza
kutowania nafasi hiyo, ni kuwataka wanachama wengine wenye mapenzi na Yanga
wajiandaye kuiwinda nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika
Juni mwaka huu na kurithi mikoba yake.
Mengi
yanasemwa wakati huu. Wapo wanaosema uamuzi wa Manji umetokana na kuchoka
mwenendo mbaya wa wanachama wake wa kuishi kwa kubangaiza kutoka kwake.
Wengine
wanasema kuwa uamuzi wake umetokana na kushindwa kuisaidia Yanga kama
alivyotangaza hapo awali.
Inawezekana
ni kati ya sababu nilizotaja zimemfanya Manji asite kuendelea kuwa mwenyekiti
wa Yanga, ila mwisho wa siku lazima tujuwe Yanga ina wanachama wengi.
Sio Manji
tu, mtu yoyote anaweza kuwania nafasi hiyo, hivyo kinachotakiwa ni mapenzi, moyo
wa uthubutu na malengo ya kuisaidia klabu ya Yanga.
Hakika
siwezi Kuvumilia. Hii ni baada ya kuona wanachama wa Yanga wanajidanganya kuwa
Manji atakuwa mwenyekiti wa milele. Hii sio kweli hata kidogo na lazima wadau
hawa wapingwe.
Wanaojidanganya
kuwa Manji anafaa kuwa mwenyekiti miaka yote, hawajui wajibu wao. Kwanini sasa
wampigie magoti? Asipokuwapo Manji, Yanga haitakuwapo?
Wanampigia magoti
hata pale alipotangaza kusimama kwa ajili ya kuwaachia wengine waongoze na yeye
kufanya biashara zake? Hapo ndipo unaposhangaa Yanga.
Yanga ni
kati ya timu zenye wanachama na wapenzi wengi. Wana kila sababu ya kuwa timu
tajiri kama watakuwa na moyo wa uzalendo na mbinu nzuri za kuendesha kibiashara.
Mtaji wa
wanachama wanao. Sasa kwanini washindwe kujua wajibu wao? Kwani Manji ndio
nani? Hakika siwezi kuvumilia na jambo hili linashangaza Dunia.
Hata yeye huenda
anawacheka Yanga. Anajiuliza, hawa wanaonipigia magoti wana mawazo sahihi?
Baada ya kuwaza na kujiuliza, atapata jibu kuwa wanampigia magoti ili maisha
yao yaendelee.
Wanajua
watavuna chochote kitu, ukizingatia kuwa ndio hao hao wanaopitisha hoja za
migogoro klabuni hapo ili wapate visenti vya kula wao na familia zao.
Hakika
siwezi kuvumilia. Ni wazi Yanga na klabu zote zinastahili kujiendesha kwa
mipango kwa kutumia rasilimali watu na rasilimali fedha na kuacha kuwa tegemezi
miaka nenda rudi.
Baada ya
kusema hili, naamini huu ni wakati wa wanachama wa Yanga kujiandaa kumpongeza
Manji kwa uzalendo wake na nia yake ya kupisha wengine waongoze itakapofika
Juni mwaka huu katika Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo.
Na wale
wanaona kuwa Manji amefanya makosa sana kupisha wengine basi wajuwe wao ni
wadhaifu na vitendo vyao hivyo vinaweza kufifisha maendeleo, wakidhani hoja zao
zinaweza kuwa na mashiko, wakati zimekuja maalum kuneemesha matumbo yao.
+255
712053949
No comments:
Post a Comment