KIKOSI cha Twiga Stars kinashuka
Uwanja wa Nkoloma, Lusaka nchini Zambia leo kuwavaa wenyeji Zambia
(Shepolopolo) katika mechi ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC)
itakayooneshwa moja moja ‘live’ na televisheni ya Shirika la Taifa la
Utangazaji la Zambia (ZNBC).
Mechi hiyo itaanza saa 9 kamili
mchana kwa saa za Zambia ambapo Tanzania itakuwa saa 10 kamili jioni huku Kocha
Mkuu wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage akiwa tayari ametangaza ‘silaha’ zake kwa
mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza.
Watakaoanza kupeperusha bendera ya
Tanzania katika mechi hiyo ambayo kiingilio ni bure kwa majukwaa yote isipokuwa
lile kuu ni; Fatuma Omari 1, Fatuma Bashiru 17, Donisia Daniel 2, Fatuma Issa
5, Evelyn Sekikubo 15, Sophia Mwasikili 16, Vumilia Maarifa 10, Mwapewa Mtumwa
9, Asha Rashid 14, Etoe Mlenzi 13 na Shelida Boniface 7.
Wachezaji wa akiba ni Maimuna Said
18, Fatuma Hassan 12, Zena Khamis 6, Esther Chabruma 8, Amina Ally 4, Therese
Yona 11 na Happiness Hezron 3.
No comments:
Post a Comment