TIMU ya Mbeya City imeshindwa kuutumia uwanja wake wa
nyumbani wa Sokoine, mjini Mbeya, baada ya kulazimishwa sare na Simba SC,
katika mechi iliyomalizika kwa kufungana bao 1-1.
Bao la Mbeya City lilifungwa na Deogratius Julius dakika ya 14, wakati Simba
walisawazisha kwa kupitia Amis Tambwe, dakika ya 50. Kwa ujumla mchezo ulikuwa
na ushindani, ambapo pia kunyesha kwa mvua ndani ya uwanja huo ulisababisha
wachezaji kuteleza uwanjani.
Mbeya City watabidi wajilaumu sana kwa kushindwa kutoka na ushindi mbele ya Simba, ukizingatia kuwa wao walikuwa na sababu zote za kushinda kutokana na maandalizi yao sambamba na ari ya vijana wao.
Matokeo hayo hayana tofauti na siku walipocheza na Yanga, ambapo zilitoka sare ya bao 1-1 katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, katika mfululizo wa Ligi ya Tanzania Bara.
No comments:
Post a Comment