Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WINGA wa timu ya Yanga, Mrisho
Ngassa na mshambuliaji wake Emmanuel Okwi, ndiyo wachezaji wanaoogopwa na wachezaji
wa timu ya Komorozine ya nchini Comoro, watakapokutana kesho Jumamosi, katika
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Dalaam, ikiwa ni mbio za Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mechi hiyo ya kwanza katika
michuano hiyo, inaanza huku Yanga wakitumainiwa kuvuka raundi ya pili kutokana
na uwezo wa wachezaji wake dhidi ya vijana hao wa Comoro.
Akizungumza jana jijini Dar es
Salaam, Nahodha wa timu ya Komorozine, Er Feda Rohaned, alisema kuwa wamekuwa
na shauku sana ya kumdhibiti Ngassa na Okwi ili wasilete madhara katika mechi
yao ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Alisema kuwa wanafahamu ubora
halisi wa Ngassa na namna ya kukabiliana naye ndani ya uwanja katika mchezo wao
muhimu wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa.
“Tunamuhofia Ngassa na Okwi
kwasababu ni wachezaji wazuri na wenye uwezo wa kufanya makubwa uwanjani,
lakini sisi tumejipanga kukumbana nao.
“Tunaamini wachezaji wote wa Komorozine
tutafanya kazi kwa bidii kuwania ushindi dhidi ya Yanga, ambayo inaanza katika
uwanja wa nyumbani kwao dhidi yetu,” alisema.
Wacomoro hao wanaanza kwa mkosi
wa kukumbana na Yanga yenye kila dalili ya uchu wa ushindi katika mechi hiyo
muhimu ili ifuzu hatua ya pili ya michuano hiyo ya Kimataifa.
No comments:
Post a Comment