Na Mwandishi Wetu, Handeni
MKUU wa wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, amesema kwamba ni
aibu kubwa kwa wilaya yake kuomba chakula lich licha ya kuzalisha chakula kingi
kwa mwaka.
Akizungumza na Handeni Kwetu Blog wilayani hapa, Rweyemamu
alisema kuwa hali hiyo inampa wakati mgumu, maana wao ni miongoni mwa wilaya
zinazoheshimika katika kuzalisha zao la mahindi.
Alisema wafanyabiashara wengi wanaingia Handeni kununua
mahindi, hivyo ni wakati wao sasa kuliangalia jambo hilo kwa kina na kuleta
tija.
“Kwanza lazima tupige vita kuuza mahindi bila kuweka akiba
yetu na familia zetu, maana huo ni mpango mbaya unaotufanya tuombe chakula kila
mwaka.
“Nikienda mjini kuomba omba chakula napata wakati kwasababu
tuna ardhi ya kutosha na wakulima wetu wengi wanalima, ila mwisho wa siku
wanauza hadi akiba za kula wao na watoto wao,” alisema Rweyemamu.
Kwa mujibu wa Rweyemamu, wananchi wote na wakazi wa Handeni
wanapaswa walime sana, huku wakijiwekea akiba badala ya kuuza chakula chao,
hivyo kuifanya wilaya hiyo ikumbwe na njaa kila wakati.
No comments:
Post a Comment