Na Mwandishi
Wetu, Mwanza
KAMPUNI ya
Bia Tanzania(TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari Lager jana imetoa mafunzo
kwa wachoma nyama kutoka Baa mbali mbali
za Mkoa wa Mwanza ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya Safari Nyama Choma kwa
mwaka 2014 yatakayo fanyika katika viwanja vya Furahisha.
Jaji Mkuu wa Safari Lager Nyama Choma, Lawrence Salvi
Akizungumza na
waandishi wa habari, Meneja matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kanda ya Ziwa,
Erick Mwayela, alisema lengo la kutoa mafunzo ni kutoa elimu kwa wachoma nyama
ukizingatia uchomaji nyama ni moja
sehemu ya kujiingizia kipato katika Bar.
Mwayela alisema
kutokana na hali hiyo wakaona ni vema wakaendesha Semina kwa wachoma nyama ili
waweze kukidhi vigezo vya mahitaji ya Wateja ili waweze kufurahia Nyama choma
kama ilivyo kwa vyakula vingine ili kuendana na kauli Mbiu ya Bia ya Safari
Lager isemayo“ Safari Lager bila nyama choma haijakamilika.”
Aliongeza
kuwa baada ya mafunzo hayo yaliyotolewa kwa Baa 37 ambao wametunukiwa vyeti vya
ushiriki pia kutakuwa na mashindano ya kuchoma nyama ambapo washindi 10
watapatikana kutokana na watakaofuzu vigezo na masharti waliyopewa katika
semina hiyo.
Alisema
Fainali za Mashindano zitafanyika Machi 9, Mwaka huu katika Viwanja vya Furahisha
ambapo washindi watapewa zawadi kuanzia mshindi wa kwanza atakayejinyakulia
Shilingi Milioni moja na Kikombe, mshindi wa pili Laki nane, Mshindi wa tatu
Laki 6, Mshindi wa nne laki nne na Mshindi wa Tano shilingi laki mbili huku
mshindi wa Sita hadi wa Kumi watajinyakulia kifuta jasho cha shilingi 50,000/=.
Alisema
namna ya kuwapata washindi ni kutokana na wateja kupiga kura katika utaratibu
utakaobandikwa katika Baa shiriki ambapo mteja atapiga kura kupitia simu ya
mkononi ili kuichagua baa inayochoma nyama vizuri.
Aliongeza
kuwa baada ya zoezi hilo kukamilika katika Mkoa wa Mwanza itaendelea katika
Mikoa mingine ambayo ni Kilimanjaro,Arusha na Dar Es Salaam, mikoa ambayo
imetajwa kuwa ndiyo vinara wa uchomaji nyama pamoja na kuongoza kwa mauzo ya
bia ya Safari Lager tofauti na maeneo mengine.
Kwa upande
wake Mkufunzi wa Mafunzo hayo, Laurence Salvi ambaye pia ni Jaji Mkuu wa mashindano
hayo amesema huwezi kuandaa mashindano bila ya kutoa Elimu, hivyo TBL
wamefikiria jambo la msingi sana lenye manufaa kwa waandaaji yaani wachoma
nyama mpaka kwa watumiani yaani mlaji.
Bwana
Lawrence binfsi aliishukuru TBL kupitia bia ya Safari Lager kufikiria jambo
zuri la kufadhili elimu kwa kwa wachoma nyama jambo ambalo si faida kwa wachoma
nyama tu bali hata watumiaji sasa watakula nyama inayostahili.
No comments:
Post a Comment