https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Sunday, November 17, 2013

Yanga: Hatutasajili kwa presha


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

UONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema kwamba hautafanya usajili kwa presha katika kikosi chao katika msimu wa usajili wa dirisha dogo unaoendelea.

Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto, pichani.
Yanga juzi ilifanikisha kuipata saini ya kipa wa zamani wa Simba, Juma Kaseja, usajili uliopokewa kwa hisia mbili tofauti juu ya mlinda mlango huyo mahiri.


Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema kwamba usajili ni jambo linalohitaji umakini na sio kukurupuka.


Alisema kwa kushirikiana na viongozi na benchi la ufundi, wanaamini kila kitu kitakwenda sawa, kwa ajili ya kuwa na timu nzuri katika mzunguuko wa pili na michuano ya Kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Hatuwezi kufanya usajili wa presha ukizingatia kuwa tunakabiriwa na michuano migumu, hivyo lazima tuwe na timu imara yenye uwezo wa kufanya maajabu,” alisema Baraka.


Yanga imemaliza mechi za mzunguuko wa pili huku ikiwa kileleni kwa pointi 28, ikifuatiwa na timu ya Azam FC yenye pointi 27, ambapo kwa sasa timu zote zinapigania kuboresha vikosi vyao katika usajili wa dirisha dogo.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...