https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, November 01, 2013

Clouds Media Group kudhamini tamasha la Handeni

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Clouds Media Group, imekuwa miongoni mwa wadau waliojitokeza kudhamini Tamasha la Handeni, linalotarajiwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu na kusubiriwa kwa hamu wilayani Handeni mkoani Tanga nchini Tanzania.
Mkurugrnzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.
Kwa sasa maandalizi kabambe yamekuwa yakipamba moto kwa ajili ya kuhakikisha kuwa tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza katika historia ya Taifa kwa mafanikio makubwa, sanjari na kutafuta mbinu za kimaendeleo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo linalotambulika pia kama ‘Handeni Kwetu’, Kambi Mbwana, alisema kuwa kuingia kwa kampuni hiyo ni sehemu ya kulifanya tamasha hilo liwe na mvuto mkubwa zaidi.

Alisema kuwa juhudi zao ni kuhakikisha kuwa tamasha hilo linafanyika wilayani humo na kushirikisha mkoa wa Tanga na Tanzania kwa ujumla, hivyo ni wakati wa wadau wengine kujitokeza kuliwekea mguso wazo hilo.

“Tunashukuru kuona Watanzania wote wanaingia humu ili wazo hili lifanikiwe kwa kiwango kikubwa, ingawa tamasha hili linafanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu, huku likiwa na changamoto lukuki.

“Naamini huu utakuwa mwanga mzuri kutoka kwa wenzetu Clouds Media Group ambao pia wanamiliki redio ya Clouds FM na Clouds TV, huku wakiwa ni waandaaji wa Tamasha kubwa la Fiesta linalofanyika kila mwaka na kuzunguuka mikoa mbalimbali ya Tanzania na kukonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa ndani na ule wa Kimataifa,” alisema Mbwana.

Wadhamini wengine ni Yusuphed Mhandeni, ambaye ni Mchumi wa CCM Kata ya Makumbusho kwa kupitia Kampuni yake ya Phed Trans, Grace Products, Screen Masters na mtandao wao wa Saluti5.com, Dullah Tiles & Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, PLAN B SOLUTIONS (T) LTD,  Country Business Directory (CBD) na Michuzi Media Group.

Wengine ni duka la mavazi la Chichi Local Ware, Smart Mind & Arters chini ya Anesa Company Ltd, ikidhamini kwa kupitia kitabu chao cha ‘Ni Wakati Wako wa Kung’aa’, Lukaza Blog, Kajunason Blog, Jiachie Blog na Taifa Letu.com.



No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...