Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
RAIS wa Shirikisho la
Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi, amevitaka vilabu vya soka vya Simba na Yanga
kukubali matokeo ya uwanjani ili wasiingie kwenye mgogoro kwakuwa ofisi yake
watakuwa wakali dhidi yao.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi, pichani.
Malinzi aliyasema hayo katika makabidhiano ya ofisi kutoka kwa rais aliyemaliza muda wake, Leodgar Tenga, huku yakihudhuriwa na watu mbalimbali kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo la aina yake.
Malinzi aliyasema hayo katika makabidhiano ya ofisi kutoka kwa rais aliyemaliza muda wake, Leodgar Tenga, huku yakihudhuriwa na watu mbalimbali kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo la aina yake.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Malinzi alisema watakaokiuka
sheria zitawabana, huku akitumia muda mwingi kuwataka Simba na Yanga wakubali
matokeo na kuacha kufanya vurugu.
Alisema yoyote atakayefanya mambo kinyume sheria hazitawaacha
watambe, hivyo mchezo wowote utakapokuwa unafanyika mwamuzi ndiyo anakuwa mtu
wa mwisho kwenye patashika hiyo.
“Sisi wote ni mashuhuda katika tukio la kufanya vurugu ndani
ya uwanja, mechi ya Simba na Kagera Sugar, hivyo lazima tujuwe kuwa hata
sekunde za mwisho za mchezo wowote, bado
mwamuzi ndio mtu wa mwisho.
“Naomba niseme kuwa tutakuwa wakali katika suala lolote
litakalofanywa kinyume, hivyo nadhani dawa ni kwa timu kujiandaa vizuri badala
ya kusubiri lawama kwa waamuzi na kufikia kuvunja viti,” alisema Malinzi.
Watu mbalimbali walihudhuria katika hafla ya makabidhiano hayo,
akiwamo Mwenyekiti wa Baraza la Michezo BMT Dioninz Malinzi, Meya wa Manispaa
ya Ilala, Jery Silaa na wengineo.
No comments:
Post a Comment