https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Wednesday, November 06, 2013

Matukio katika picha juu ya semina ya wenyeviti wa kata za Kinondoni, mjini Dodoma inayoendelea

Mjumbe wa NEC, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi, akisisitiza alipozungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kikazi ya siku tatu kwa wenyeviti wa CCM wa kata 31 za wilaya ya Kinondoni, jana, Nov 5, mjini Dodoma. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Dodoma Albert Mgumba na kulia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Dodoma mjini, Saad Kusilawe na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge. (Picha na Bashir Nkoromo).
Mwenyekiti wa CCM, wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge, akimshukuru Dk. Rehema kwa kufungua mafunzo hayo.

Washiriki wakishangilia baada ya mafunzo hayo kufunguliwa rasmi na mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dk. Reheme Nchimbi.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo maalum kwa wenyekiviti wa CCM Kata za Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, baada ya kufungua semina yao jana mjini Dodoma.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi akiagana na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge baada ya kufungua semina ya Wenyeviti wa CCM Kata zote za wilaya ya Kinondoni, DSar es Salaam, jana mjini Dodoma.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...