Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA wa ngumi za kulipwa hapa
nchini, Francis Cheka, amesema kwamba umaarufu wake unampa uchungu kwasababu
hauendani na maisha halisi anayoishi kutokana na mchezo huo kutawaliwa na njaa
ya kutisha.
Bondia Francis Cheka, pichani.
Akizungumza jana kwa njia ya simu
akitokea mkoani Morogoro, Cheka alisema mfumo mzima wa maisha yake umekuwa wa
njaa na hakuna kampuni inayofikiria namna ya kuingia naye mkataba ili afike
mbali zaidi.
Alisema amekuwa akipata fedha
kiduchu mara chache anapokuwa na pambano, huku gharama za maandalizi za mchezo
huo kuwa kubwa na kumpa wasiwasi wa maisha yake ya baadaye atakapoachana na
masumbwi.
Cheka alisema ukata huo ndio
unaomfanya ashindwe kutembelea kaatika mikoa mbalimbali ya Tanzania kujionea
hali ya masumbwi ilivyo sanjari na kushirikiana na wadau wengine kuweka mipango
ya kimaendeleo.
“Hakika hali hii inanipa wasiwasi
mkubwa, maana wakati mwingine maisha yanakuwa magumu na inashangaza kwanini
nakuwa maarufu wakati ukata umeshika hatamu, hivyo suala hili linanipa wakati
mgumu.
“Naomba wadau wa masumbwi na kampuni
kuingia sasa kunisaidia, ukizingatia kuwa naandikwa na kutajwa mno, ilaa vipi
thamani ya umaarufu wangu inaendana na maisha halisi ninayoishi ndani na nje ya
masumbwi,” alisema.
Cheka ni miongoni mwa mabondia
mahiri wanaotamba kwa kiasi kikubwa katika mchezo wa masumbwi, huku kila
anayeingia naye ulingoni akifanikiwa kuibuka kidedea na kuitangaza nchi katika
kona za Kimataifa.
No comments:
Post a Comment