https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, November 05, 2013

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga awaagiza watendaji kusimamia miradi ya maendeleo kwa ukaribu

Na Amina Omari, Tanga.
Mwenyekiti wa Chama Chama Mapinduzi Wilaya ya TangaKassim Mbuguni pichani, watendaji wa mitaa,vitongoji na kata kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo kwa ukaribu katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama hicho  na kama wakishidwa waachei ngazi.

Agizo hilo alilitoa wakati wa uzinduzi wa shina la Vijana wa nguvu kazi wa  Chama Cha Mapinduzi UVCCM kata ya  Mzizima mwishoni mwa wiki ambapo alisema kuwa haiwezekani kuwa na watendaji ambao hawasimami wa kutekekeleza ilani ya chama.

Alisema kuwa ifike mahali ni lazima tuwe na watendaji ambao tunaendanao kwenye maamuzi yetu sio kuwa na ambao wanatupinga na kurudisha nyuma maendeleo pamoja na kasi katika kuwasogezea huduma wananchi. “Salamu nazitoa kwa watendaji ambao watashindwa kusimamia na kutekeleza miradi wajitoe wenyewe,Ni aibu kwa mtendaji wa mtaakushindwa kusimamia mradi mdogo wa darasa moja la shule halafu unajiita mtendaji hutufai katika mbio zetu za kuleta maendeleo jitoe
mapema kabla hatujakutoa kwa nguvu”Mbuguni.

Pia aliwashauri watendaji hao kuacha kukaa ofisi pekee na kusubiri taarifa kwenye makaratasi bali wahakikishe wanashuka hadi katika ngazi za chini za wananchi na kusikiliza kero zinazowakabili ili kuzitafutia ufumbuzi wa haraka .

Aliongeza kuwa sifa ya kiongozi bora aliyechaguliwa na wananchi ni kuhakikisha anawasikiliza na kuwatatulia kero zao wanazokabilianazo waliomchangua na sio kusubi maamuzi kutoka ngazi za juu pekee.

“Nawapa taarifa nitaanza kupita kuanzia ngazi za mitaa,kata na vitongoji katika Jiji hili na  kukagua maendeleo na changamoto zilizopo Na jinsi zilivyotatuliwa na viongozi wa serikali nitakapo baini mapungufu hatabaki mtu nitamtoa kwa aibu “alisisitiza Mbuguni.


Katika Hatua nyingine alimuagiza Diwani wa Kata hiyo Daniel Mgaza  kuhakikisha na maliza kabisa changamoto ya ukosefu wa maji na umeme katika kata hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu ili wananchi hao wasiendelea kuteseka na kero hizo.

Alisema kuwa diwani ni ndio msimamiaji sera na ndiuo aetetea wananchi katika kata yake hivyo tatizo la maji na umeme kuikabili kata hiyo tena ipo mjini ni jambo la aibu hivyo ni vemna ahakikishea ameimaliza mapema kero hiyo.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...