Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BENDI za
TwangaPepeta, Msondo Ngoma na wanamuziki kibao kutoka Sikindeni sehemu ya wasanii
watakaosindikiza tamasha kubwa la Gurumo 53 litakalofanyika mwezi huu.
Muhdini Gurumo, pichani.
Tamasha
hilo ambalo ni mahsusi kwa ajili ya kumuaga mwimbaji mkongwe Muhidi Maalim Gurumo
litafanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe Jumamosi
ya tarehe 14. Kwa mujibu
wa kamati ya watu sita inayoratibu tamasha hilo, Gurumo anaagwa baada ya kutangaza
rasmi kuachana na muziki wa jukwaani baada ya kudumu kwenye kazi hiyo kwa miaka
53.
Mratibu
wa kamati hiyo Juma Mbizo amesema kutakuwa pia na wasanii wa bongo fleva,
vichekesho na sarakasi. Aidha Mbizo
amesema tamasha litatanguliwana bonanza la soka la maveterani. Hadi kustaafu
kwake Gurumo aliyezitumikia pia bendi za Kilimanjaro Chacha, Rufiji Jazz, Kilwa
Jazz, Sikindena OSS – Ndekule, alikuwa ni kiongozi na mmoja wa wamiliki wa Msondo
Ngoma ambayo hapo awali ilijulikana kwa majina ya NUTTA, Juwata na OTTU. Gurumo
ameitumika Msondo katika majina yote ya nyuma.
Wasanii
waliowahi kuitumikia Sikinde ambao watakuwepo kumsindikiza Gurumo ni pamoja na Cosmas
Chidumule, Abdallah Gama, Hussein Jumbe, Mashaka Shaaban, Kalamazoo, Henry
Mkanyiana Karama Legesu.Wengine ni Ali Yahayana Boniface Kachala, Benno Villa
Anton, Tshimanga Kalala Assossa na Ibrahim Mwinchande.
Baadhi ya
wasanii wengine watakaotumbuiza ni Komandoo Hamza Kalala, Kassim Mapili, Hafsa Kazinja
na Waziri Ali. Kamati ya
Gurumo iko chini ya uenyekiti wa Asha Baraka, makamuni Waziri Ali na katibu ni
Said Mdoe huku mratibu akiwa Juma Mbizo, wajumbe ni Said Kibiriti na Richardson
Sakala.
No comments:
Post a Comment