https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Tuesday, November 12, 2013

Ally Mustafa Barthez atoa la moyoni sakata la Kaseja kusajiliwa Yanga

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

MLINDA mlango wa Yanga, Ally Mustafa ‘Barthtez’, amesema kwamba hatima ya maisha yake ya soka kwa sasa ipo mikononi mwa klabu yake ya Yanga, huku akisema kuwa hana wasiwasi kwa kusajiliwa Juma Kaseja katika klabu yao.

Kipa wa Yanga, Ally Mustafa Baerthez, pichani.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Barthez alisema kwamba bado ana mkataba halali na klabu yake hiyo ya Yanga, hivyo wao ndio wenye kujua nini cha kufanyaa, kabla ya yeye kuchukua uamuzi sahihi.


Alisema kwamba ujio wa Kaseja katika timu hiyo hauna shaka mioyoni mwake, kwakuwa wote wapo katika timu moja, hivyo suala la ushindani au mwingine kuuzwa au kutolewa kwa mkopo ni jambo la kawaida katika mpira wa miguu.

“Nimesajiliwa kihalali Yanga nab ado nina mkataba ndani ya timu hii, hivyo lolote linaloweza kutokea kwa wakati huu nimejiandaa nalo na siwezi kuogopa kucheza na Kaseja au mimi kuuzwa katika klabu nyingine.


“Haya ni matokeo ya kawaida katika suala zima la mpira wa miguu duniani kote, hivyo siwezi kupata hofu kwa lolote na nimejiandaa vizuri katika hilo,” alisema.

Barthez aliwahi kuwekwa benchi kwa misimu kadhaa na Kaseja walipokuwa timu moja ya Simba, jambo ambalo lilisababisha Barthez ahamie Yanga, kabla ya kipa huyo mwishoni mwa wiki iliyopita kusajiliwa Yanga kwa miaka miwili

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...