Na Rahimu Kambi, Dodoma
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho
Kikwete, amewashangaa majirani zake, nchi za Kenya, Uganda na Rwanda kwa
kufanya vitendo vinavyoashiria ubinafsi na kuitenga nchi ya Tanzania, bila
sababu za msingi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Jakaya Mrisho Kikwete, pichani.
Rais Kikwete aliyasema hay oleo mjini Dodoma alipokuwa
akilihutubia Bunge, ikiwa ni miaka kadhaa tangu alipofanya hivyo mwishoni mwa
mwaka 2010 alipozindua Bunge hilo lilipotoka katika Uchaguzi Mkuu.
Akizingumza kwa hisia kali, Kikwete alisema kwamba pamoja na nchi hizo kutaka
kuitanga nchi yake, ila Tanzania itaendelea kuipenda Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) na kamwe haitaweza kuondoka, licha ya dalili za ubinafsi wa
Kenya, Uganda na Rwanda kuongezeka.
Rais Kikwete alisema kwamba wao kama wakuu wan chi wamekuwa
wakikutana na kubadilisha mawazo ya kuinga jumuiya hiyo, hivyo inashangaza
kuona wapo watu wanaotaka kufanya mambo yanayoshangaza kwa mustakabali wan chi za
Afrika.
"Inashangaza kama kuna watu wanaona sisi hatufai kuwa kwenye
makubaliano ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, ukizingatia kuwa tunatumia
gharama kubwa katika bajeti yetu kutenga mambo ya Jumuiya hii.
"Na kama wenzetu kuna kosa tumelifanya, nadhani njia nzuri
ingekuwa kuwa wawazi na sio kufanya mambo ambayo si mazuri kwa mustakabali wan
chi zetu,” alisema Rais Kikwete na kuongeza Tanzania itaendelea kuwa kwenye
jumuiya hiyo na kamwe hawatakuwa tayari kutoka.
Awali Rais Kikwete pia alitumia muda huo kuzungumzia juhudi
za kupambana na majangili Tanzania na duniani kote ili kuweka mkakati sahihi wa
kuzuia majangili wanaongamiza rasilimali za Tanzania, wakiwamo wanyama aina ya
faru na tembo pamoja na mbao.
Pia alizungumzia mchakato wa kuelekea kwenye Katiba Mpya,
akisifia taratibu zote zilizotumika hadi kufikia wakati huu ambapo rasimu ya
kwanza imepatikana, huku siku chache zijazo wakitarajiwa kupatikana wajumbe wa
Bunge la Katiba.
No comments:
Post a Comment