Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilaya Kinondoni, kimeanza mikakati
ya kuwanoa viongozi wake ili kuwapatia uzoefu wa kukitumikia chama kwa kipindi
kijacho na hatimae kuwa na nguvu, kwa kuandaliwa semina itakayofanyika kesho (leo),
mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM wilaya Kinondoni, Salum Madenge, akiwa kwenye moja ya matukio ya kichama.
Semina hiyo inahusu wenyeviti wa CCM wa Kata zilizopo wilayani Kinondoni, huku ikiwa na dhamira yaa kuhakikisha viongozi hao wanapewa uwezo wa kutimiza majukumu yao ya kila siku.
Semina hiyo inahusu wenyeviti wa CCM wa Kata zilizopo wilayani Kinondoni, huku ikiwa na dhamira yaa kuhakikisha viongozi hao wanapewa uwezo wa kutimiza majukumu yao ya kila siku.
Akizungumza leo asubuhi wakati viongozi hao wanaelekea
katika semina hiyo ya siku nne mjini Dodoma, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Kinondoni, Salum
Madenge, alisema kwamba siku zote malengo ya chama ni kushika dola, hivyo
anaamini kwa kuandaliwa semina hiyo ni sehemu ya kujenga mfumo mzuri wa
kiutendaji ndani ya chama chao.
Alisema ukiacha semina ya wenyeviti wa Kata Kinondoni, pia
Makatibu wameshafanyiwa mpango huo, jambo ambalo linaonyesha mwendo mzuri wa
chama chao.
“Chama chetu kina mwingiliano mzuri wa kiungozi na changamoto
mbalimbali, hivyo utaratibu wa semina kwa viongozi wake ni mzuri kwakuwa
unawapa nafasi ya kujitathimini mahali walipo na wanapoelekea.
“Tunaahidi kuwatumikia Watanzania wakati wowote kwa
kuhakikisha kuwa kuanzia ngazi ya chini ya viongozi wetu hadi Taifa wanafahamu
wajibu wao na malengo ya kuwasimamia wananchi,” alisema Denga.
Semina hiyo imeandaliwa na CCM Kinondoni kwa kushirikiana kwa
karibu na Mchumi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Makumbusho, Yusuph Mhandeni
kwa ajili ya kuwapa mbinu mbalimbali wenyeviti hao ili waje kukitumikia chama
kwa juhudi na maarifa.
No comments:
Post a Comment