https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Monday, November 11, 2013

Wananchi waja juu marehemu kuingizwa kwenye orodha ya mihutasari ya mapato na matumizi wilayani Handeni mkoani Tanga

Rajabu Athumani, Handeni
WANANCHI wa kijiji cha Taula kata ya Kwedizinga wilaya ya Handeni mkoani Tanga wameshangaa kukuta orodha ya majina ya watu waliofariki katika mihutasari ya mapato na matumizi ya mkutano wa kijiji hali ambayo ilileta sintofahamu miongoni mwao.

Wakihoji suala hilo katika mkutano wa kijiji uliofanyika wiki iliyopita, wanakijiji hao Rashid Kiwanda alisema waligundua kuingizwa kwa majina ya watu ambao walifariki mwaka 1996 hadi 1997 lakini walikuwemo kwenye orodha ikimaanisha kuwa nao walihudhuria kikao hicho kitu ambacho sio kweli.

Walitaja majina ya marehemu hao kuwa ni, Zuberi Husein ambae alifariki mwaka 1996, mwalimu Hemed Omari aliyefariki mwaka 1997 na wengine wengi kitendo ambacho kiliwashangaza wananchi hao.

“Taarifa hii ilisomwa marabaada ya wanakijiji kulalamika kwa mtendaji kata kuwa wamekaa miaka mitatu bila kusomewa taarifa hiyo, ndipo mtendaji kata alipo amuru isomwe, katika mihutasari hiyo ya mapato na matumizi pia yaliwekwa majina ya marehemu waliokufa miaka mingi iliyopita mfano mzuri na marehemu mwl Hemed Omari aliyefariki mwaka 1997, Zuberi Husein mwaka 1996 na wengine wengi,”alisema Kiwanda.

Mtendaji wa kijiji hicho wa sasa Mohamedi Mbwana alikiri kuwepo kwa majina hayo katika muhtasari huo wa na kudai kuwa aliyeweka majina hayo katika mahudhurio sio yeye ila ni mwenzio ambao kwasasa hayupo na tayari taarifa hizo imepelekwa ngazi za juu kwa hatua zaidi kwa kugushi mahudhurio ya mkutano.

“Hilo suala lakuwekwa majina ya watu waliofariki katika orodha ya wananchi waliohudhuria kikao hicho ni kweli na jukumu hilo nimemuachia mtendaji wa kata alisema kuwa suala hilo atalipeleka ngazi za juu kwaajili ya hatua zaidi”alisema Mbwana.

Aidha pia wananchi hao wamelalamikia kitendo cha baadhi ya viongozi wa kijiji kuwapa maeneo wawekezaji bila ya kuwashirikisha wananchi na kusema kuwa kuna baadhi ya wawekezaji hawakujadiliwa na kijiji lakini wamepewa maeneo isivyo halali.

Hata hivyo mtendaji huyo wa kijiji Mohamedi Baraka alisema kuwa katika kijiji chake kuna wawekezaji sita na miongoni watano wamepitishwa kihalali ila mmoja ndio wananchi walimkataa na taratibu za kuhalalisha zinaendelea kama itawezekana.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...