Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema
kwamba benchi la ufundi chini ya Kocha wao Ernest Brandit, alipendekeza Juma
Kaseja kusajiliwa ndani ya kikosi chao, jambo lililofanikiwa baada ya kuingia
naye mkataba wa miaka miwili.
Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto, pichani.
Usajili wa dirisha dogo wa Kaseja kwa timu ya Yanga, umepokelewa kwa hisia kali na mashabiki wa soka wa Tanzania, huku uongozi ukionekana kupongeza kwa nyota huyo kujiunga na timu yao kwa ajili ya mzunguuko wa pili.
Usajili wa dirisha dogo wa Kaseja kwa timu ya Yanga, umepokelewa kwa hisia kali na mashabiki wa soka wa Tanzania, huku uongozi ukionekana kupongeza kwa nyota huyo kujiunga na timu yao kwa ajili ya mzunguuko wa pili.
Akizungumza jana jijini Dar es
Salaam, Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema kwamba ni kweli wameingia
naye mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia klabu yao.
Alisema hatua ya kumsajili nyota
huyo imetokana na mahitaji ya kocha wao aliyetaka kumnyakua kipa huyo mwenye
uwezo mahiri wa kusimama langoni kwa umakini.
“Viongozi wa Yanga wanafanya
usajili kwa kupewa nafasi na benchi la ufundi, hivyo walipomuhitaji Kaseja
ndio taratibu zikafuatwa.
“Kaseja ni kipa mzuri hivyo tunaomba
wanachama na mashabiki wa Yanga kumpokea kwa mikono miwili kwa ajili yaa
kuitumikia timu yetu katika michuano ya mzunguuko wa pili na Ligi ya Mabingwa
Afrika, baadaye mwakani,” alisema.
Awali alipoulizwa juu ya suala la
kusajiliwa Kaseja, Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako alionyesha
kupingana na madai hayo, akisema si kauli za viongozi.
“Acheni kusikiliza maneno kutoka
vichochoroni huko, badala yake msikie kauli za viongozi, maana mengi
yataendelea kusikika zaidi ya hayo ya Kaseja kusajiliwa na Yanga,” alisema.
No comments:
Post a Comment