Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na tukio la kuvamiwa na kushambuliwa Dk
Sengondo Mvungi, Mjumbe wa Tume ya Katiba. Waziri Nchimbi alisema
upepelezi wa tukio hilo umefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 80 ambapo
tayari watuhumiwa tisa wamekamatwa wakiwa na mapanga na simu moja ya
mkononi, watuhumiwa hao walitajwa majina yao katika mkutano huo
uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini
Dar es Salaam leo. Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na
waandishi wa habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi likiendelea na
uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine. Kushoto ni Naibu
Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Kulia ni Kamishna wa Polisi
Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova. Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam,
Suleiman Kova akiwaonyesha waandishi wa habari mapanga waliyoyakamata
wakati wa msako mkali wa kuwasaka watuhumiwa waliomvamia na kumshambulia
Dk Sengondo Mvungi Mjumbe wa Tume ya Katiba. Katika msakao huo
watuhumiwa tisa walikamatwa wakiwa na mapanga na simu moja ya mkononi.
Katikati (waliokaa meza kuu) ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame
Silima. Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa
habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi
kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine. Mkutano huo ulifanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini
Dar es Salaam leo.
Sehemu ya waandishi
habari waliohudhuria mkutano wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi alipokuwa anazungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali
vya habari vya nchini na nje ya nchi kuhusiana na tukio la kuvamiwa na
kushambuliwa Dk Sengondo Mvungi, Mjumbe wa Tume ya Katiba. Waziri
Nchimbi alisema upepelezi wa tukio hilo umefanikiwa kwa zaidi ya
asilimia 80 ambapo tayari watuhumiwa tisa wamekamatwa wakiwa na mapanga
na simu moja ya mkononi, watuhumiwa hao walitajwa majina yao katika
mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba
wananchi na waandishi wa habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi
likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment