Na Fadhili Athumani, Moshi
KLABU ya vijana ya mchezo wa Riadha ya Holili (HYAC),
imetuliwa kuwa kituo cha kutoa fomu za ushirki wa mbio za Uhuru Marathon zitakazofanyika
kuanzia Desemba 8 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Mratibu wa Uhuru Marathon 2013, Innocent Melleck akizungmza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) |
Akizungumza hilo, Mkurugenzi wa HYAC
ambayo imeanza kujizoloea sifa kwa kuzalisha na kuendeleza wanariadha
wanaotamba katika riadha hapa nchini, Domician Rwezaura, aliyabainisha hayo leo.
Rwezaura alisema kutokana na mafanikio ambayo Klabu
yake imekuwa ikipata hivi karibuni katika mashindano mbalimbali ambayo wanariadha
wake wamekuwa wakishiriki, Waandaaji wa Uhuru Marathon, kupitia mratibu wa
Mashindano, Innocent Melleck imeiomba klabu hiyo kuwa kituo cha kuchukulia fomu
za ushiriki wa mbio hizo kwa mji wa Moshi na maeneo ya jirani na Mkoa wa Kilimanjaro.
“Ndio hawa jamaa walitufuata na kutuomba kusimamia
zoezi la utoaji wa fomu kwa miji ya Moshi na maeneo ya jirani na mkoa wa Kilimanjaro
na tayari tumeshapata ofisi pale stendi kuu ya Mabasi nah ii ni kutokana na
ukweli kwamba Holili ni mbali sana,” alisema Rwezaura.
Rwezaura alisema fomu hizo zitapatikana katika Ofisi
zao zilizoko katika jengo la Plaza, mkabala na stendi ndogo ya mabasi
yanayofanya safari kwenda Rombo, Marangu na Mwika.
Kwa upande wake, Mratibu wa Mbio za Uhuru Marathon,
Innocent Melleck, akizungumza na gazeti hili kwa njia ya Simu
kutoka Dar es salaam, alisema taratibu za kuhakikisha fomu za usajili
zinapatikana katika kituo hicho zimeshafanyika na kwamba zitaanza kutolewa
kwanzia Ijumaa ya ya wiki hii.
“Ni kweli tutatumia klabu hiyo kama kituo chetu kwa
mji wa Moshi na Maeneo ya jirani kwa ajili ya upatikanaji wa fomu za usajili,
tumeshawasiliana na Mkurugenzi wao na ametuhakikishia ushirikiano wao kama
wadau wa mchezo wa Riadha” alisema Melleck.
No comments:
Post a Comment