Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MPACHIKA mabao mahiri wa timu ya
Simba, Hamis Tambwe, amesema amemaliza ligi akiwa na uchungu kwa kushindwa
kuonyesha cheche zake alizotarajia katika mzunguuko wa kwanza wa Ligi ya
Tanzania Bara.
Akizungumza jijini Dar es Dalaam
juzi, Tambwe alisema kuwa alikuwa na hamu ya kuiweka kileleni timu yake kwa
kufunga mabao mengi zaidi, ukiacha bao 10 alizofanikiwa.
Alisema jambo hilo linamfanya arudi
kwenye mzunguuko wa pili akiwa na uchu wa kuwa kinara wa kupachika mabao katika
mechi za mzunguuko wa pili zitakazoanza January mwakani.
“Nimefanya kila niwezalo ili nifunge
mabao mengi zaidi uwanjani, lakini nimefanikiwa kupata bao 10 na kufuatiwa na
Elius Maguli wa Ruvu Shooting mwenye bao 9.
“Msimu ujao nitakuwa mkali zaidi
kwakuwa nitaendelea na mazoezi hata nje ya michuanio ya Ligi, maana sijapenda
niwe kinara kwa mabao machache,” alisema Tambwe.
Tambwe ambaye ni raia wa Burundi,
ndio anayeangaliwa kwa umakini zaidi na mashabiki wa Simba wakiamini kuwa
anaweza kuipaisha klabu yao na hatimae kunyakua ubingwa.
No comments:
Post a Comment