https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Monday, November 18, 2013

Chuo cha Polisi Moshi mabingwa wa judo

Na Mwandishi wetu, Moshi
KLABU ya Mchezo wa Judo chuo cha taaluma ya polisi Moshi (MPA)  imefanikiwa kuchukua ubingwa wa jumla katika mashindano ya kwanza ya  mchezo huo yaliyofahamika kama First Moshi Polisi Academy Judo Championship 2013.
Bingwa wa mchezo wa judo Afrika mashariki Geofrey Mtawa wa magereza Ukonga akijaribu kutaka kumtupa mchezaji Abubakary Magogo wa MPA katika pambano la wazi ambalo hata hivyo Mtawa alipoteza kwa pointi.
Katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na Chuo cha Polisi kwa  kushirikana na chama cha mchezo wa Judo nchini ilishuhudiwa wachezaji  chipukizi kutoka vilabu vya Korogwe, Kisutu  na Moshi Polisi
wakionesha vipaji vyao huku mchezaji wake chipukizi, Andrew Thomae  akiibuka mchezaji bora wa mashindano.
Klabu ya Moshi Polisi ilifanikiwa kuibuka mshindi wa baada ya  wachezaji wake kutawala mapambano ya uzito wa kilo 60, 66, 73 pamoja na mapambano ya wazi yaani Open huku klabu ya Korogwe ikifanikiwa
kushika nafasi ya pili.
Mchezaji Thomae  wa MPA ambaye ndiye chachu ya ubingwa wa MPA, alianza kuonesha ubabe wake mbele ya mpinzania wake Dola Abeid ambaye pia anatoka klabu ya MPA akimwangusha mara kadhaa ndani ya dakika 3:34:05 za mchezo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza wa mchezo wa Judo Geofrey Mtawa wa magereza Ukonga kwa wachezaji wa uzito wa kilogramu 90.
Thomae pia alifanikiwa kumbwaga mchezaji Abubakar Magogo katika mchezo wa fainali ambaye awali alimduwaza bingwa wa Judo  Afrika mashariki Geofrey Mtawa kutoka klabu ya magereza Ukonga katika hatua ya nusu fainali mchezo ambao hata hivyo uliisha kwa Mtawa kurusha lawama kwa muamuzi kuwa hakutendewa haki. 

Akizungumza jana jijini hapa, baada ya mchezo kumalizika, Mtawa alisema kuwa kimsingi alichokifanya mwalimu wake ni kinyume na sheria za mchezo kwani alimnyima pointi za wazi ambazo zingepelekea yeye kutangazwa mshidni kwa kile alichodai kuwa Mwamuzi huyo kuwabeba “Madogo”.
Mchezaji bora wa mchezo wa Judo katika mashindano ya First Moshi  Poilisi Academy Judo Championship 2013,Andrew Thamae akiwa ameshikilia  vikombe alivyo fanikiwa kutwaa, kulia kwake ni kamanda wa polisi mkoa  wa Kilimanjaro Robert Boaz aliyekuwa mgeni rasmi.
“Huu ni uonevu, pale kilichotokea ni uonevu, mimi nimetumia tekniki za mchezo nimemnyanyua dogo ndani ya uwanja nikamwangusha chini tena ameangukia mgongo lakini cha kushangaza mwamuzi ananinyima pointi eti nimenyanyua nje ya uwanja, hapana mchezo huu hautakuwa kwa staili hii, wananishushia hadhi yangu,” alisema Mtawa.
Washindi wengine katika mapambano mengine ni Bakari Magogo kilo 60 (MPA), Mohammed Korogombe kilo 73 (MPA), Gervas Chilipueli, kilo 81 (Korogwe), Amina Mohammed mpambano wa wazi (MPA) na Geofry Mtawa kilo 90.
Zawadi katika mashindano kwa mshindi wa kwanza katika uzito wa 60 hadi 90 ni vyeti, vikombe, medali na fedha taslimu ambapo washindi wote walizawadiwa zawadi zao na mgeni rasmi Kamanda wa Polisi Mkoani
Kilimanjaro, ACP-Robert Boaz.
Mashindano hayo yalidhaminiwa na Mkuu wa Chuo cha MPA, Matanga Mbushi kwa kushirikiana na kampuni ya  Marenga Investment, Ibra Line, Tanzanite One, pamoja na Benki ya NMB tawi la Mandela .

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...