https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Monday, November 25, 2013

Katibu Mkuu CCM, Abdulrahman Kinana awasili Kyela kwa Meli


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiri (kulia), wakishuka kutoka katika mv Songea, baada ya msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kuwasili katika bandari ndogo ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24, 2013.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi, baada ya kuwasili katika bandari ndogo ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24, 2013.
Nahodha wa mv Songea Tom Faya akimpatia maelekezo ya namna meli hiyo inavyofanya kazi, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, wakati katibu mkuu huyo alipokuwa akisafiri na meli hiyo kutoka Mbamba Bay mkoani Ruvuma kwenda Kyela mkoani Mbeya, leo Nov 24, 2013. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Siasa na Uhisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro. Kwenye usukukani ni Nahodha Msaidizi, Conrad Shauritanga.
Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe akimlaki wa furaha, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipompokea katibu mkuu huyo, baada ya kuwasili katika bandari ndogo ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
Baadhi ya abiria waliosafiri na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana katika mv Songea, alipokuwa alitokea Mbamba Bay mkoani Ruvuma kwenda Kyela mkoani Mbeya. Meli hiyo iliyoanza kazi katika Ziwa Nyasa, mwaka 1974, ina uwezo wa kubeba abiria 213 wakiwemo wafanyakazi 13 wa meli hiyo. (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO).

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...