https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, November 21, 2013

Kinana asema CCM haiwezi kurubuni ili chama chao kipate kura

 Balozi Hilda Komba wa shina namba 9 Tawi la Amani Makolo akimkaribisha  nyumbani kwake Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na wanachama wa shina namba 9,katika tawi la Amani Makolo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa kijiji cha  Aman Makolo waliojitokeza nyumbani kwa Balozi Hilda Komba wa shina namba 9 ,Tawi la Amani Makolo wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma.
 Wanachama wapya wa Tawi la Amani Makolo wilayani Mbinga wakila Kiapo cha  Uanachama wa CCM mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana   ambaye leo amefanya ziara katika wilaya ya Mbinga.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na wanachama wa Shina namba 9 Tawi la  Amani Makolo ambapo aliwapongeza kwa ushirikiano na mshikamano waliokuwa nao kiasi wameweza kuwa na wanachama hai 426.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakazi wa kijiji  cha Mtundawalo wakati akiwasili kijijini hapo tayari kwa kufanya mkutano wa hadhara.Katika Mkutano wa hadhara Katibu Mkuu wa CCM alizungumzia  mipango mbali mbali ya kutatua matatizo ya wananchi na kuwaeleza  wananchi CCM haiwezi kurubuniwa  kwa sababu ya kupata kura,akasisitiza  wananchi wawe wa kweli kwa serikali ili haki itendeke kwa haraka.


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na viongozi wengine 
wa CCM kulima shamba la wanawake na vijana wajasiriamali Mkwaya kata ya  Kilimani.


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajasiriamali wa  Mkwaya kata ya Kilimani ambao kwa pamoja wameamua kujishughulisha na  kilimo.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akiwasalimu wakulima wa kata ya Mkwaya .
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia ngoma ya Mganda wakati akiwasili kwenye eneo la mkutano wilayani Mbinga.
 Katibu wa NEC Itikadi na uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mbinga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya michezo Mbinga mjni.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya  kukabidhi pikipiki 50 zilizotolewa na mbunge kwenda kwa watendaji wa  vijijini.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimueleza Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose uzoefu wake wa kuendesha   pikipiki,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbinga  Ndugu Senyi Ngaga.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Mbinga  mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanika kwenye viwanja vya michezo  vya Mbinga mjini ambapo aliwaeleza wananchi kuwa chama cha Mapinduzi  kitasaidia kutoa ushauri kwa mazao ambayo bei yake inashuka na kupanda.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa Wilaya wa zamani Ndugu Osmund Kapinga.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Mzee Osmund Kapinga Mkuu wa Wilaya mstaafu mara baada ya kukamilika  mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya michezo  vya Mbinga mjini mkoa wa  Ruvuma.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...