Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAZIRI wa Viwanda na Biashara ambaye pia ndio mbunge
wa Handeni, Dkt Abdallah Kigoda, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la
Utamaduni, lililopangwa kufanyika Katika Uwanja wa Azimio, wilayani Handeni
mkoani Tanga, Desemba 14 mwaka huu.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt Abdallah Kigoda, pichani.
Tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza wilayani hapa,
huku likitarajiwa kuwa la aina yake kutokana na maandalizi yanayoendelea
kushika kasi.
Akizungumza jana mjini Handeni, Mratibu wa Tamasha hilo,
Kambi Mbwana, alisema maandalizi yamezidi kushika kasi kwa kuangalia mazoezi ya
vikundi kadhaa vitakavyotoa burudani katika tukio hilo.
“Tunashukuru Mungu kuona mambo yanazidi kuwa mazuri kwa
kuhakikisha kuwa Desemba 14 mwaka huu tunafanya tamasha lenye mguso na kila
mmoja wetu kufaidishwa.
“Huu ni wakati wa kila mtu kujipanga ili aje kushiriki kwa
namna moja ama nyingine, ukizingatia kuwa juhudi hizi zote zipo kwa ajili ya
kujenga ushirikiano kwa watu wote,” alisema Mbwana.
Wadhamini katika tamasha hilo ni pamoja na gazeti la Mwananchi,
Clouds Media Group, ni Phed Trans, Clouds Media
Group, Grace Products, Screen Masters na mtandao wao wa Saluti5.com, Dullah
Tiles & Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, PLAN B SOLUTIONS
(T) LTD, Country Business Directory (CBD) na Michuzi
Media Group duka la mavazi la Chichi Local Ware, Smart Mind & Arters
chini ya Anesa Company Ltd, ikidhamini kwa kupitia kitabu chao cha ‘Ni Wakati
Wako wa Kung’aa’, Lukaza Blog, Kajunason Blog, Jiachie Blog na Taifa Letu.com,
huku likipangwa kuanza saa 2 za asubuhi hadi saa 12 za jioni.
No comments:
Post a Comment