Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete
akiongozwa na Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kukagua
daraja la Mwanhuzi lililoko Meatu Mkoani Simiyu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete
akiongozwa na Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kukagua
daraja la Mwanhuzi lililoko Meatu Mkoani Simiyu.
Muonekano wa Daraja la Mwanhuzi.
Ahadi
ya ujenzi wa daraja la Mwanhuzi katika wilaya ya Meatu mkoani Simiyu
imetimia baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya
Kikwete kulifungua rasmi daraja hilo ambalo ujenzi wake umekamilika na
tayari limeanza hutumika.
Awali
kabla ya kulifungua daraja hilo Rais Kikwete aliwaasa wananchi wa eneo
hilo la Mwanhunzi pamoja na watumiaji wengine kulitunza daraja hilo ili
liweze kudumu kwa muda uliokusudiwa na hivyo kuhakikisha panakuwepo
huduma hiyo muhimu ya usafiri kati ya Wilaya ya Meatu na Mikoa ya jirani
ya Arusha na Singida.
‘Ninawasihi
mlitunze daraja hili na asije akatokea mtu kwenda kuanza kukata vyuma
au kunyofoa vifaa vingine vya daraja kwani kwa kufanya hivyo
mtalidhoofisha ubora wake na hatimaye kuharibika kabisa tukajikuta
tunarusi katika kero ya usafiri katika eneo hili kama ilivyokuwa hapo
awali kabla ya kujengwa kwa daraja” Alisisitiza Rais kikwete .
Aidha,
Mhe. Rais aliongeza kuwa atahakikisha katika kipindi cha miaka miwili
kilichobakia akishirikiana na Waziri Magufuli watahakikisha wanafikisha
sehemu nzuri ahadi zote za miradi ya barabara katika wilaya hiyo na mkoa
wa Simuyu kwa ujumla.
Daraja
la hilo lenye urefu wa meta 40 ni kiungo muhimu cha usafiri kuvuka mto
Mwanhuzi ambako barabara kuu inayo tokea Kolandoto mkoani Shinyanga
kupitia Lalago katika mkoa wa Simiyu na kuelekea mikoa ya Singida na
Arusha.
Awali
wakati akimkaribisha Rais, Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli alielezea kuwa usanifu pamoja na usimamizi wa daraja hilo
umefanywa na Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) kwa gharama ya
Shilingi milioni 13.45 na ujenzi wake umetekelezwa kwa awamu mbili.
”Kukamilika
kwa mradi huu ni moja ya ushahidi unaothibitisha kuwa ahadi ulizotoa
kwa wananchi zinakamilika popote bila kuangalia itikadi za vyama au
watu” alisema Waziri Magufuli
Waziri
Magufuli alifafanua kuwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa daraja hilo
ilikamilika mwezi Agosti mwaka 2013 ikiwa imejengwa na Mkandarasi M/S
Pet Cooperation kutoka Kahama kwa gharama ya Shilingi milioni 355.58.
Awamu
ya pili ya mradi huu ambazo zilianza mwezi Agosti 2013 na kukamilika
nwezi Oktoba 2013 zilijumuisha ujenzi wa kingo za daraja. Kazi hizo
zillitekelezwa chini ya usimamizi wa Ofisi ya Meneja wa Tanroads mkoa wa
Simiyu mara baada ya mkoa huo mpya kuanzishwa. Awamu hii ya pili
ilitekelezwa na Kampuni ya Ms Tolerance Engineering Ltd ya Dar es Salaam
kwa gharama ya Shilingi milioni 97.55.
Fedha
hizo zote zilizotumika katika ujenzi wa awamu zote mbili pamoja na
usimamizi ambazo ni jumla ya Shilingi milioni 455.58 zimetolewa na Mfuko
wa Barabara (Roads Fund).
No comments:
Post a Comment