WABUNGE wanaoiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki wamesema suluhisho la matatizo ya nchi za Maziwa Makuu yatapata ufumbuzi wa kudumu iwapo kutakuwa na utaratibu wa kukaa meza moja kwa pande zote husika na kufanya mazungumzo ya kuleta amani.
Mwenyekiti
wa Wabunge wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA),Adam Kimbisa
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati
wabunge hao wakitoa pongezi kwa Rais Jakaya Kikwete kwa hotuba yake
aliyoitoa Bungeni hivi karibuni. Kushoto ni Katibu wa Wabunge
hao, Shy-Rose Bhanji.
wanahabari wakifuatilia hotuba hiyo..
Mwenyekiti
wa Wabunge wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA),Adam Kimbisa
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati
wabunge hao wakitoa pongezi kwa Rais Jakaya Kikwete kwa hotuba yake
aliyoitoa Bungeni hivi karibuni. Kushoto ni Katibu wa Wabunge
hao, Shy-Rose Bhanji. Kulia ni Mkurugezni Msaidizi wa MAELEZO, Zamaradi
Kawawa.
Hayo
yalisemwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa wabunge hao, Adam
Kimbisa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam
ambapo pia alipongeza hotuba ya Rais Jakaya Kikwete alioitoa Bungeni
Dodoma Novemba 7 mwaka huu juu ya Jumuiya hiyo.
“Sisi
tunaamini amani ni jambo la msingi katika Afrika Mashariki na hasa
katika nchi zilizo katika Maziwa Makuu. Tunawapongeza wanajeshi wetu na
wanajeshi Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa kazi nzuri walioifanya
iliyowezesha mafanikio kupatikana” alisema.
Akielezea
juu ya baadhi ya nchi wanachama wa EAC ambao ndio waanzilishi wa vurugu
mbalimbali na migogoro Mwenyekiti huyo alisema kuwa Tanzania imekomaa
kisiasa hivyo hawawezi kuwaondoa wale wanaoleta chokochoko kwa kuwa dawa
ni kuzungumza na sio kuwatoa.
Mtangamano Aidha Kimbisa amesema misingi ya Utengamano wa kiuchumi ikijengeka vizuri na kufanya kazi ipasavyo wananchi wote wa Afrika Mashariki watafaidika na hivyo suala la kuruka hatua yoyote ni jambo lisilokubalika.
“Tunaungana
na kauli ya Rais kwamba Tanzania ni kati ya nchi zinazotaka ngazi zote
za mchakato wa Mtangamano zitekelezwe moja baada ya nyingine bila kuruka
hatua yoyote. Hatua ya kwanza ni Umoja wa Forodha inafuata soko la
Pamoja kasha Umoja wa Fedha na hatimaye shirikisho la Kisiasa” alisema.
Alisema
hadi sasa ni hatua mbili zilizotiwa saini na mchakato wa kuweka saini
Umoja wa fedha unatarajiwa kutiwa saini baada ya kikao cha Juu cha
Marais kinachotarajiwa kufanyika mjini Kampala Novemba 30 iwapo masuala
yote muhimu ya mchakato huo yatakuwa yamekamilika.
“Jambo
la msingi ambalo hata Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya imesema wazi
kwamba Jumuiya lazima iwe ni ya wananchi kwa manufaa ya wananchi na
isiwe ya viongozi. Wananchi washirikishwe katika kila hatua na kila
ngazi ili iweze kushiriki kikamilifu kwa ajili ya maslahi yao” alisema.
Kuhusu VISA alisema kuwa wao wanaruhusu nchi nyingine kuendelea lakini Tanzania bado hawajafikia muafaka kwa kuwa wanaangalia maslahi ya nchi kwanza. Katika Hatua nyingine, Wabunge hao walimpongeza Rais Kikwete kupeleka kikosi cha Wanajeshi katika Brigedia Maalum iliyoundwa na Umoja wa Mataifa ili kuongeza nguvu ya kudhibiti waasi Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
No comments:
Post a Comment