https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, November 29, 2013

Wakongwe kibao waipania shoo ya Gurumo Desemba 14

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKONGWE wamuziki  wa  dansi  Kassim  Mapili amethibisha kushiriki Tamasha la Gurumo 53 litakalofanyika Jumamosi ya tarehe 14 mwezi Disemba mwaka huu.
Mapili amesema siye yetu, bali pia ataratibu mpango mzima wa kuhakikisha wakongwe wote wamuziki wa dansi wanashiriki tamasha hilo bure bila malipo yoyote.
Mwanamuziki mkongwe, Muhidin Gurumo
Tamasha hilo ambalo ni mahsusi kwa ajili ya kumuaga mwimbaji mkongwe Muhidin Maalim Gurumo litafanyika fcJijini Dar es Salaam katikaviwanjavya TCC Club Chang’ombe.

Mratibuwatamashahilo,  Juma Mbizo amesema Mapili ameamua kubeba jukumu la kuandaa wakongwe ambao ambao watatengeneza wimbo maalum wakumuaga Gurumo utakaosikika kwa mara ya  kwanza TCC Club Disemba 14.

Baadhi ya wakongwe wengine waliothibitsha kushiriki Tamasha  la Gurumo 53 ni pamoja Komandoo Hamza Kalala, Tshimanga Kalala Assossa na Waziri Ali.
Gurumo anaagwa kufuatia kutangaza kwake kuacha na rasmi na muziki wajukwaa ni baada ya kudumu kwenye kazi hiyo kwa miaka 53.

Bendi za Twanga Pepeta, Msondo Ngoma na wanamuziki kibao waliowahi kung’ara na Sikinde ni sehemu ya wasanii watakaosindikiza tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu.
Hadi kustaafu kwake Gurumo aliyezitumikia pia bendi za  Kilimanjaro Chacha, Rufiji  Jazz,  Kilwa Jazz, Sikinde na  OSS – Ndekule,  alikuwa nikiongozi na mmoja wa wamiliki wa Msondo Ngoma.

Wasanii waliowahi kuitumikia Sikinde ambao watakuwepo kumsindikiza Gurumo ni pamoja na Cosmas Chidumule,  Abdallah Gama, Hussein Jumbe, Mashaka Shaaban,  Kalamazoo, Henry Mkanyia na Karama Legesu. Wengine ni  Ali  Yahaya na Boniface Kachale, Benno Villa Anton na Ibrahim Mwinchande.

Hata hivyo, licha ya wasanii hao waliowahi kuitumikia Sikinde kuwemo kwenye tamasha hilo, bendi ya Mlimani Park “SikindeNgomaya Ukae”  haitashirki katika Gurumo 53 kutokana sababu zilizo nje ya uwezo wao.

Mbizo amesema Mlimani Park inamkataba unaowabana kufanya onyesho lolote litakalowakutanisha na Msondo hadi baada ya sikukuu ya Krismasi (Disemba 25, 2013).
Juma Mbizo amesema licha ya Sikinde kutoshiriki tamasha hilo lakini nyimbo zote zilizotamba ndani ya bendi hiyo ambazo zilitungwa na Gurumo, zitarindima TCC Club kwa ubora ule ule.

“Wanamuziki wengi waliofanya kazi na Gurumo katika Sikinde enzi hizo, hawa kote na katika bendi hiyo, hivyo watakuwa huru kuungana na mwimbaji huyo mkongwe na kushusha burudani nzito.


No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...