https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Monday, November 11, 2013

Extra Bongo, Jakaya Arts dimbani
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
NYASI za uwanja wa shule ya msingi Ubungo jijini Dar es Salaam leo zinatarajiwa kuwaka moto wakati timu ya wanamuziki wa bendi ya Extra Bongo na kundi la Sanaa ya Maigizo la Jakaya watakaposhuka dimbani kumenyana katika mechi ya kirafiki maalumu kwa ajili ya kuzindua 'Extra Bongo Funs'. 
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa bendi hiyo Juma Kasesa, maandalizi ya mchezo huo yamekamilika ambapo kwa wiki kadhaa sasa vikosi vya timu zote vimekuwa kwenye mazoezi makali kujiwinda na mchezo unaovuta hisia za mashabiki wa soka waliokamia kumuona Mkurugenzi wa Extra Bongo Kamarade Ally Choki akicheza beki wa kati (mkoba). 

Aliwataja baadhi ya nyota wa bendi hiyo watakaoshuka dimbaniwakiongozwa na nahodha wao Salum Chakuku 'Chakuku Tumba' kuwa ni Athanas Muntanabe, Super Nyamwela, Redo Mauzo, Efraim Joshua, Adam Hassan, Hosea besi, Danger Boy, Adam Bombole na Ally Koncho ambao wameapa kuadhibu wapinzani kutokana tambo nyingi ambazo wamekuwa wakizitoa dhidi yao. 

Kwa upande Mkurugenzi wa Jakaya Arts linalorusha mchezo wake katika kituo cha runinga cha ITV kila Jumamosi, Devid Mponji, alisema, wamejiandaa vya kutosha kuikabili Extra Bongo na kwa kiwango cha safu yake ya ushambuliaji Choki atakuwa uchochoro wa kuruhusu kufungwa mabao mepesi kwakuwa hatoweza kumudu kasi waliyonayo. 

Alisema, kikosi chake kinanolewa na kocha wa timu ya Kijogoo maarufu kwa jina 'Kikoti' chini ya nyota wake Erick Mikongoti, Rashid Mawala, Omary Zero na nahodha Jose Mawala.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...