https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, November 01, 2013

Kamishna wa Magereza Tanzania, John Casmir Minja akabidhi vyeti vya udereva kwa mafunzo ya maaskari magereza

image 
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(mbele katika Jukwaa) akipokea Saalam ya heshima na Utii kutoka kwa Gadi Maalum ya Gwaride lililoandaliwa na Wahitimu 72 wa Mafunzo Maalum ya Udereva katika Chuo cha Magereza cha Ufundi na Udereva Kingolwira, kilichopo Mkoani Morogoro. Hafla fupi ya ufungaji Mafunzo hayo imefanyika leo Novemba 1, 2013 katika viwanja vya Kingolwira, Morogoro.
2 

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja  (kulia) akikagua Gadi Maalum ya Gwaride lililoandaliwa Maalum kwa ajili ya Ufungaji Mafunzo ya Udereva Kozi No. 19 ya Mwaka 2013 ambayo yamefanyika leo Novemba 1, 2013 katika Chuo cha Magereza cha Ufundi na Udereva Kingolwira, Mkoani Morogoro. 3 
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kushoto) akikagua moja ya Gari aina   Bedford ambalo hutumika kufundishia Madereva Wanafunzi katika Chuo cha Magereza cha Ufundi na Udereva kilichopo Kingolwira, Mkoani Morogoro. Mafunzo Maalum ya Udereva yamefungwa rasmi leo Novemba 1, 2013 na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini.
4 
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja akimkabidhi cheti mmoja wa Wahitimu wa Kozi ya Udereva, Cpl. Nuru kutoka Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salaam. Cpl. Nuru ni minongoni mwa askari 11 wa Kike ambao wamehitimu mafunzo Maalum ya Udereva leo Novemba 1, 2013  na Mafunzo hayo yamefanyika kwa muda wa Mwezi mmoja katika Chuo cha Ufundi na Udereva Kingolwira, Mkoani Morogoro ambapo jumla ya Askari 72 wamehitimu Mafunzo hao kwa ustadi mkubwa.
5 
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(aliyesimama) akitoa hotuba fupi ya ufungaji Mafunzo Maalum ya Udereva leo Novemba 1, 2013 katika Chuo cha Magereza cha Ufundi na Udereva Kingolwira, Mkoani Morogoro.
6
Baadhi ya Askari wa Jeshi la Magereza ambao wamehitimu Mafunzo Maaalum ya Udereva katika Chuo cha Magereza cha Ufundi na Udereva Kingolwira, kilichopo Mkoani Morogoro wakisikiliza hotuba ya Mgeni Rasmi. Mafunzo hayo Maalum ya Udereva yamefungwa rasmi leo Novemba 1, 2013 na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(hayupo pichani).
6 
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Askari wa Kike Wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Udereva(waliosimama) mara baada ya hafla fupi ya ufungaji Mafunzo Maalum ya Udereva yaliyofanyika Chuo cha Udereva Kingolwira, Mkoani Morogoro leo Novemba 1, 2013( wa nne toka kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa( wa nne toka kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Naibu Kamishna wa Magereza, James Selestine(wa pili toka kushoto) ni Asha Said, Afisa Tarafa Mikese, Morogoro(wa tatu toka kushoto) ni Diwani wa Kata Mkambalani, Morogoro Kamishna Msaidizi wa Magereza Mstaafu, Daniel Shawa. Wengine walioketi ni Bwana Fedha Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Gideon Nkana(wa pili kulia) na wa tatu kulia ni Mkuu wa Chuo cha Ufundi na Udereva Kingolwira, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Osmund  Nduguru(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...