https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Sunday, November 17, 2013

Stars sasa kukipiga na Zimbabwe Jumanne ijayo Uwanja wa Taifa

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
TIMU ya Taifa, Taifa Stars sasa inacheza na Zimbabwe mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA Date itakayofanyika keshokutwa Jumanne (Novemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura.
Awali Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilikuwa icheze na Kenya (Harambee Stars), lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF) lilituma taarifa jana jioni (Novemba 16 mwaka huu) likieleza kuwa timu yake haitacheza tena mechi hiyo.


Kikosi cha Zimbabwe chenye msafara wa watu 30 kinatarajia kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kesho (saa 3 asubuhi) tayari kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 11 kamili jioni.


Waamuzi wa mechi hiyo wanatoka Uganda wakati Kamishna atakuwa Leslie Liunda wa Dar es Salaam. Mwamuzi wa mezani ni Oden Mbaga pia wa Dar es Salaam.


Stars chini ya Kocha Kim Poulsen ipo kambini tangu Novemba 12 mwaka huu kujiwinda kwa mechi hiyo. Kim amejumuisha kwenye kikosi chake wachezaji watano wanaocheza mpira wa miguu nje ya Tanzania.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...