Na Mwandishi Wetu, Handeni, Tanga
MKUU wa
wilaya Handeni, DC Muhingo Rweyemamu, amewataka wananchi wa Handeni, mkoani
Tanga kulitumia Tamasha la Handeni kwa ajili ya kutafuta fursa za kimaendeleo.
Mkuu wa Wilaya Handeni, mkoani Tanga, Muhingo Rweyemamu, pichani.
Akizungumza
jana mjini Handeni, Muhingo alisema kutokana na tamasha hilo kufanyika mwisho
wa mwaka, Desemba 14, itakuwa chachu ya kuwaunganisha watu wote, sanjari na
kujadili changamoto zinazoikabiri Handeni na Tanzania kwa ujumla.
Muhingo alisema
kuwa tamasha hilo lina umuhimu mkubwa kutokana na kuandaliwa maalum kwa ajili
ya Watanzania kwa ajili ya kuangalia ngoma na matukio mbalimbali ya kijamii.
“Wakati
napongeza kwa dhati kuandaliwa kwa tamasha hili wilayani hapa, pia nawaomba
watu waje kwa wingi kushuhudia namna gani Handeni imepiga hatua kimaendeleo na
kuangalia namna gani wanaweza kusonga mbele.
“Naamini
tutafikia hatua nzuri kwa kushirikiana na wadau wote, hivyo wale wanaoishi
mbali na Handeni pia ni wakati wao kurudi nyumbani mwishoni mwa mwaka kujifunza
mambo ya utamaduni wao, sanjari na kufanya juhudi za kupiga hatua kimaendeleo,”
alisema.
Tamasha hilo
linaloandaliwa na Mratibu wake Kambi Mbwana, hadi sasa limedhamiwa na Phed Trans, Clouds Media
Group, Grace Products, Screen Masters na mtandao wao wa Saluti5.com, Dullah
Tiles & Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, PLAN B SOLUTIONS (T) LTD, Country Business Directory (CBD) na Michuzi Media Group.
Wengine ni duka la mavazi la Chichi
Local Ware, Smart Mind & Arters chini ya Anesa Company Ltd, ikidhamini kwa
kupitia kitabu chao cha ‘Ni Wakati Wako wa Kung’aa’, Lukaza Blog, Kajunason
Blog, Jiachie Blog na Taifa Letu.com, huku likipangwa kuanza saa 2 za asubuhi
hadi saa 12 za jioni.
No comments:
Post a Comment