Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
PIGO limetokea katika muziki wa taarabu kufuatia kifo cha
mwimbaji wake Nyawana Fundikira aliyefariki leo jijini Dar es Salaam,
akisumbuliwa ugonjwa wa malaria uliosababisha kifo chake na kupokewa kwa
uchungu na wadau wote.
Marehemu Nyawana Fundikira mamaa Matashtiti enzi za uhai wake, akiwa ndani ya kundi la T-Moto Modern Taarab. Mwimbaji huyu amefariki Dunia leo jijini Dar es Salaam.
Wadau wa taarabu wamepokea kwa masikitiko makubwa kutokana
na kifo cha mwanadada huyo aliyeimba wimbo wa Domo la Udaku akiwa na kundi la
T-Moto, lililokuwa linamilikiwa na Amin Salmin Amour.
Mume wa marehemu, Kais Mussa Kais alithibitisha kutokea kwa
kifo cha mke wake na kusema kuwa msiba huo umekuja, huku ukimuachia majonzi
makubwa.
Taarifa zaidi za msiba huo zitaendelea kuwajia kadri zitakavyoendelea
kupatikana, ambapo kwa sasa mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya
Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment