Na Masanja Mabula -Pemba
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Shekhan Mohammed Shekhan amewapongeza
wachezaji wa timu ya Polisi inayoshiriki ligi kuu Visiwani hapa kwa
kuonyesha nidhamu na kucheza kwa kujituma na kufanikiwa kuchukua alama
sita kutoka Kisiwani Pemba .
Akizungumza
na msafara wa timu hiyo huko Ofisini kwake
Wete , Kamanda Shekhan amewataka wachezaji na viongozi wa timu hiyo
kuongeza juhudi za mazoezi ili kuiwezesha timu kuchukua moja ya nafasi
za juu kwenye msimamo wa ligi na kuiwakilisha Nchi kwenye michuano ya
Kimataifa .
Amesema
kuwa bila ya kuwepo na ushirikiano wa dhati kati ya wachezaji na
viongozi pamoja na kuthaminiana kwa kila mmoja wawapo nje na ndani ya
uwanja mafanikio hayawezi kupatikana .
"Ni jambo la kujivunia kwamba timu umekuja Pemba na kuondoka na alama
zote sita , nawaombeni muendelee kushirikiana , kuthaminana na kupendana
ndani na nje ya uwanja ili muweze kuiletea mafanikio timu na jeshi la
Polisi Visiwani hapa," alieleza Shekhan .
Naye
msemaji wa timu hiyo Ramadhan Khamis Ramadhaman amesema kuwa ushindi
walioupata kwa mechi za Pemba umetokana na ushirikiano walionao
wachezajio pamoja na Benchi zima la uongozi ambapo kila upande ulitimiza
wajibu wake kama ilivyotakiwa.
"Unajua
mafanikio haya yametokana na sisi kuwa na ushirikiano, ambapo
wachehzaji walitekeleza majukumu yao kama walivyoelekezwa na viongozi
nao waliwajibika kwa mujibu na kazi zao," alifamaisha.
Aidha
Nahodha wa timu Adam Juma amesema kuwa lengo lao ni kutwa ubingwa wa
ligi kuu ya Zanzibar na kuwataka mashabiki na wapenzi wa timu hiyo
kuendelea
kuwaunga mkono ili waweze kutimiza azma yao hiyo .
"Lengo
ni kuwa mabingwa tumewahi kutwa ubingwa wa ligi kuu Zanzibar na
tunajua utamu wa ubingwa , sisi wachezaji tumewasha moto na kwa sasa
sifikirii kama kuna timu utauzima , tunataka kurejesha heshima na hadhi
ya timu yetu,"alijinadi Adam .
Ikiwa
kisiwani
Pemba Timu ya Polisi imecheza michezo miwili ambapo iliifunga timu ya
Kizimgbani Unioted mabao 3-1 kabla ya kuifunga timu ya Jamhuri ambayo
inahemea chumba cha wagonjwa mahtuti kwa jumla ya mabao 2-1. na kuifanya
timu ya Polis kufikisha alama 19 .
No comments:
Post a Comment