Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama
Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MAANDALIZI
ya kufanyika kwa tamasha la Wachaga yanaendelea vizuri, kwa ajili ya
kuhitimisha kwake Desemba 22 mwaka huu katika viwanja vya Ushirika Moshi,
mkoani Kilimanjaro kuanzia saa 4:00 asubuhi, ikiwa ni siku tatu kabla ya
Sikukuu ya Krismasi.
Akizungumza
na Handeni Kwetu jana, Mkurugenzi wa Kampuni ya MyWay Entertainment
Paul
Mganga, alisema tamasha hilo linalenga
kuhamasisha jamii juu ya utamaduni wa kabila hilo na mengineyo nchini.
Vilevile,
kuhamasisha jamii na familia zao zilizopo ndani na nje ya mikoa yao kukumbuka nyumbani na
kutembelea wazee mara kwa mara.
“Tuna
imani kubwa kuwa zaidi ya watu 3,000 na familia zao, watahudhuria kwa wingi
tamasha hili la kihistoria huku wakipata fursa ya kusikia historia ya kabila
la Wachagga kwa kina toka kwa wazee wanatoka kwenye familia za Machifu
naMangi Mkuu wa kabila hilo
wanaoishi mkoani Kilimanjaro.
“Kuona
na kucheza ngoma zote za asili za kichaga pamoja na vikundi tofauti tofauti vya
ngoma za asili na sanaa za makabila mengine,” alisema.
Kadhalika
kutakuwa na vyakula vya asili vya aina zote kama
kiburu, kisusio, mtori, ndafu, shiro, kiumbo, kitawa, macharari, ngararimo,
ng’ande na vingine vingi.
Pia
vinywaji vyote vya asili vya kabila hilo kama mbege, dadii
na vingine vingi.
Mganga
alitaja burudani mbalimbali zitakazokuwepo siku hiyo kuwa ni bendi ya Akudo
Impact, Msanii Mfalme Costa Siboka kutoka Dar es Salaam
na wasanii wote kutoka mikoa ya Kilimanjaro na Arusha watapamba tamasha hilo.
Katika
tamasha hilo viongozi mbalimbali wa serikali wamealikwa pia , wawekezaji na
wafanyabiashara wakubwa ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro, viongozi wa asasi
zisizo za kiserikali pamoja na asasi za serikali yetu, wakurugenzi wa makampuni
ya utalii na hoteli kubwa za mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.
Mganga
alisema wamejipanga vizuri katika kufanikisha siku za makabila yote Tanzania kila
mwaka tukianza na makabila wa kaskazini, lengo likiwa ni kuhamasisha jamii kuenzi
mila na tamaduni za makabila yetu na kukumbuka kuzipeleka familia zetu nyumbani
tuwapo nje ya mikoa yetu.
Tamasha
la Chagga Day limedhaminiwa na Safari Lager, Pepsi,
Konyagi, Precision Air, Radio 5 FM, Toyo, Samsung, Michuzi Blogspot, Zizou
Fashion, Mlonge Bi Makai, Egesha Trading Agency, CXC Africa, Delina Group
Enterprises, Linda Media Solution (LIMSO) and Albert Msando Legal Consultant.
Kiingilio ni sh.5,000 mlangoni.
No comments:
Post a Comment